SIO YULE BY SULTAN WA PWANI ft CHIKUZEE
INTRO CHORUS
Aha Si yo yo Sio yuleee..eh(sio yule)
Aha Sio yo yo Sio yulee..eh(sio yule)
Mwanamme gani hata pesa anapatiwa
Mwanamme gani hata nguo anavishwa
Mwanamme gani hata za nyumba anatumiwa
Aha Si yo yo Sio yuleee..eh (Nasema sio yule dada)
Aha Sio yo yo Sio yulee..eh
(Jichunge nae yule dada)
VERSE 1:
CHIKUZEE
Wala usiwahi kua na pupa ya mapenzi, hilo mimi nshakwambia,
Na utakuja kujuta ile kishenzi, hapo ulipo nshapitia,
Usishoboke nae katu …. Uhhh, Wasubiri wengi waja …….
Ahhh, Uhh wale washachapwa chapwa chapwa chapwa wangapi, hata wewe unajitia,
Uhh aibu yako aibu yangu, mi mwenzio nakuhurumia,
Huu mwiba unaojichoma wewe hata mimi unaniingia,
CHORUS
Aha Si yo yo, Sio yuleee..eh (sio yule)
Aha Sio yo yo, Sio yulee..eh (sio yule)
Mwanamme gani hata pesa anapatiwa
Mwanamme gani hata nguo anavishwa
Mwanamme gani hata za nyumba anatumiwa
Aha Si yo yo, Sio yuleee..eh (Nasema sio yule dada)
Aha Sio yo yo, Sio yulee..eh (Jichunge nae yule dada)
VERSE 2: SULTAN WA PWANI
Haya, hapa kaka ashasema mengi,
ila anasahau kama, Mwenye dada hakosi shemeji,
hilo ulifahamu, Kwamba hajitegemei,
hizo story ulizitoa wapi, Nawala simtetei,
ila nahisi una chuki binafsi, Haijalishi ameshachapa chapa chapa wangapi,
huenda kwake akatulia, Kila mtu ana ba ba ba bahati yake, usije ukamuharibia,
Huenda ikawa ndie yule alie mtafuta,
Hatomfanya alie, akae asiwe anajuta,
CHORUS
VERSE 3: SULTAN
Muulize, hizo pesa alimwona wapi akipatiwa,
Muulize, hizo nguo alimuona lini akivalishwa (unamuongopea)
CHIKUZEE
Usione nisemayo longo longo, ila mi nakutetea,
Huno wasia wangu ukiniskizamimi kwenye mapenzi hautopotea,
SULTAN
Na huko, kupotea ndio kuijua njia,
Una vituko, kumponda msela haitosaidia,
Apendae chongo, huita kengeza,
Umuonae ovyo, ndio amependeza,
Utamaliza kuni kwa kuchemusha mifupa na wala haivi,
Na ukitandika shemeji mangumi utalala Makupa kisha jela baridi
CHORUS
Comments
Post a Comment