EXCLUSIVE INTERVIEW: MWINYI KAZUNGU MTETEZI ATETEA SANAA YA PWANI!
Pwani Usanii: Umekua kwa industry ya muziki for long,ni wasanii wapi wa pwani unaofagilia kazi zao?
Mwinyi Mtetezi Kazungu: Wako kadhaa na sio ati ni kwa ajili ya majina.kwa mfano msanii Dogo Richie.amekuwa kwa usanii muda mfupi lakini kipaji chake hakina mfano.msanii huyu licha ya yeye kuimba peke yake kwenye vibao vyake.ameonyesha wazii kwamba ana nguvu za kuwapiku wasanii waliomtangulia na kwa kweli anaenda mbali.walioanzisha mziki pwani kama vile.nyota ndogo,ali b,cannibal na sharama,ruff daddy na ruff touch,prince adio miongoni mwa wasanii wengine hao ni vigogo.lakini kuna kina susumila,escoba,rojo mo,chikuzee,fisherman na producer totti haya ni majina yaliopo juu.
Pwani Usanii: Ahsante. Halafu wasanii wa pwani wamekuwa wakilalama sana kutopata airplay Nairobi,maoni yako ni gani kwa jambo hilo?
Mwinyi Mtetezi Kazungu: Kuna ile dhana ya kuwa wasanii kutoka pwani wako na ule uvivu flani.ingawaje mimi napinga hilo.karibuni tumeona wasanii kadhaa wakipata shows mbele ya nairobi.mfano mzuri ni msanii susumila.Ingawaje kunaeza kuwa kuna ukweli flani wa swala hili, wasanii wa mombasa wanahitaji kuekeza zaidi kwenye mziki kwani stesheni nyingi za nairobi zinahitaji miziki iliokomaa na wasanii walio na majina makubwa.Kbc hasa kupitia kipindi Top mashariki show imewapitia wasanii wa mombasa asilimia 40 ya mziki wao kuchezwa kila siku.kumaanisha mziki wa pwani unakubalika.
Pwani Usanii: Je unaweza wapa ushauri gani wasanii wa pwani wanaochipuka.
Mwinyi Mtetezi Kazungu: wajifunze kwa wasanii wakubwa humu nchini hasa wasanii wenzao pwani.wachukulie usanii kama kazi wala sio kutafuta umaarufu.watafute njia za kutoka wala wasitafute bifu zisizo na msingi,waimbe vitu vya maana vilivyo na ubunifu mkubwa na waende shule kusomea mziki ili wapate ujuzi zaidi.
Comments
Post a Comment