VIDEO MPYA YA BENSO 'PHONTO' AKIMSHIRIKISHA MISS GG.
Huku akiwa anajivunia kuwa katika anga zote za muziki wa pwani na Nairobi,msanii Benso amekaza buti zaidi na raundi hii amejitwika mzigo na kutuachia kibao kikali kwa jina 'phonto' akimshirikisha binti kwa jina miss GG.
Huku akiwa ameandaa wimbo huu kwa mtindo wa mchanganyiko wa Kwaito na Kapuka,Benso amedhihirisha uwezo mkubwa kuingia soko la muziki wa afrika mashariki. Miss GG amepamba chorus kwa sauti yake ya kuvutia na Benso kuangusha mistari mikali kwenye verse.
Video ya nyimbo hiyo iliandaliwa na Thome wa Boomba pictures huku audio ikiandaliwa chini ya studio za stantmastaz. Vilevile video ya 'phonto' ilipeperushwa kwa mara ya kwanza kwenye kipindi cha Homegrown Kbc kwenye interview na Dj Hassan.
Comments
Post a Comment