STANTMASTAZ ENTERTAINMENT YAFUNGUKA KUHUSU BEEF YAO NA LAVICHUNARE NA KUSAJILI ALI BABAZ.

 Baada ya kufanya kazi pamoja kwa muda mchache,wasanii Lavichunare na Studio ya Stantmastaz walitengana kwa njia mbaya. Lavichunare kupitia meza yetu ya habari walidai kuwa Stantmastaz recordz iliwachukua na kuwafanyisha kazi za kimuziki ili kujinufaisha. Tulipowasiliana na mmoja wa kundi hilo, alitueleza kuwa studio hio inajinufaisha kupitia jasho lao na hata kurelease kazi zao za studio zikiwa bado hazijaisha. 
Wiki chache zilizopita tulijaribu kuwasiliana na meneja wa Stantmastaz na alidai ya kuwa hizo zilikuwa porojo tu. Jana kwenye ukurasa wa facebook wa Stantmastaz ilibainika wazi kuwa maneno haya yaliwalenga lavichunare. Tukiyachukulia kama majibu na ufafanuzi wa Stantmastaz basi hatuna budi kusema kuwa Lavichunare wametupiliwa mbali na stantmastaz wamemsajili msanii mkali anayeibukia kwa jina Ali Babaz. 
Stantmastaz waliandika haya,nikinukuu kutoka kwa facebook ....."Nataka kuuliza swali... group ya wasanii wakivunjika wakawa kando kando wanaitwa nani... na hao wasanii waingie studio kila mtu siku yake na kufanya kila mtu track yake kando wanaitwa nani.. Sasa studio ina makosa gani ku release hizo track kama zimekwisha kazi yake.. na msanii moja kuja studio na kukosoa track yake na kuikubali mpaka kupanga na Mac choka video yake na mwengine akawa kimya bila mpangilio kisha kuja kulalamika sana wakati hujapanga na mwenye studio kitu.. mwanielewa lakini, sasa studio imefanya makosa kusaidia bila malipo na bila kulalamika na kuwachkua kama wetu.. ndo ukaambiwa na wahenga tenda wema uende zako maana binadamu hawana shukran... lakini bado tuko tuko kwa sana na tutaendelea kusaidia wengine wenye kutaka usaidizi wetu, wa kwanza kuwa Ali Babaz tegea muone mabadiliko... Pamoja tunaweza".

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA