KAA LA MOTO ATOA USHAURI KWA VIJANA WANAOTUMIWA VIBAYA KISIASA
Huku hali ya usalama nchini ikizidi kukumbwa na utata, mkali wa HipHop kutoka pwani Kaa La Moto amejitokeza na kutoa ushauri wake kwa vijana wanaotumika kufanya uhalifu na ugaidi.
"Sometimes mafans wanauliza, kwanini unapenda kuimba maisha au maswala ya jamii mbalimbali.Yah jibu,siwezi kuimba starehe huku sehemu kama MPEKETONI watu wanakufa,Mara nchi pia imejaa hamaki za Kisiasa na Ugaidi,hatujui yupi mkweli.#But ningesema kuwa, Wanaofanya uhalifu au kutumwa kufanya, wafanye kwa majina yao na sio kwa JINA LA DINI FLANI ili mradi uharibu Dini zingine. Nahisi kuwa labda NCHI imeuzwa na aliyeuziwa kasepa na vyeti.Nahisi Starehe imeletewa Mzungu,huku Afrika tuungane kuleta USAWA."
Comments
Post a Comment