PRODUZA AMMZ KUJIUNGA NA SIASA 2017!!!
Amepambana na uandalizi wa muziki kwa miaka kadhaa huku akiwatambulisha wasanii wakali kwenye nyanja ya sanaa ya pwani.Anaitwa produza Tone la maji au ukipenda Amz Jadidi.Produza huyu ambaye yupo ndani ya SQ recordz fununu zimejiri ya kuwa atajitosa kwenye siasa mwaka wa 2017.Amz ambaye tuliwasiliana naye pindi tu tuliposikia fununu hizo alitueleza kuwa ni kweli kuwa atajiunga na siasa mwaka wa 2017 ila bado analifikiria vizuri zaidi jambo hilo."Ni kweli kabisa kuwa nitaingia katika kiwanja cha siasa kwani wazee wangu wa sehemu ninayoishi wananipa msukumo na kunishawishi nijiunge na siasa,"Alinena Amz.Kuhusu kuacha kurekodi muziki Amz alikuwa na haya ya kusema,"Kamwe sitowacha kurekodi na kuandaa muziki,bado mimi ni produza na nitaendelea kuwa produza hata nikiwa siasani
Comments
Post a Comment