DAZLAH KUANDAA VIDEO YA 'BANGEREBA' JUMAMOSI HII.
Alianza kwa kasi na katu ameahidi kutopunguza speed yake,Kiduche almaarufu Dazlah aliyewapa vibao motomoto kama ; Dada, Shemeji, Safari Njema ,Mlevi wa Mapenzi na vingine vingi jumamosi hii atakuwa akiandaa video ya wimbo wake BANGEREBA.
Wengi waliodhani kuwa msanii huyu yupo chini ya Candy n Candy wamekosea kwani produza Tee ambaye pia ni meneja wa Dazlah alitueleza kuwa wimbo BANGEREBA upo chini ya studio ya Tee hits na video yake itaandaliwa na kampuni ya Black Merg videos,director BwoyP.Tee alitueleza hivi," ngoma itakayoandaliwa video jumamosi hii ni Bangereba anafanya na kampuni inaitwa Black Merg director anaitwa Bwoy P".
Comments
Post a Comment