LOOOOO KINGWENDU KUGOMBEA UBUNGE TANZANIA!!!!
Majina yake halisi ni Rashid Mwinshehe, na jina
lake la kisanii ni "Kingwendu". Kabila ni Mzaramo
mzaliwa wa Kisarawe. Elimu yake ni Stashahada
ya Uhasibu (Diploma in Accounting) kutoka chuo
cha Uhasibu Tanzania (TIA).
Kitaaluma Kingwendu ni Mhasibu. Amefanya kazi
ya uhasibu katika taasisi mbalimbali kabla hajaamua
kuachana nayo na kujiingiza kwenye sanaa za
maigizo ambapo anafanya vizuri katika sanaa za
vichekesho (Physical and Character Comedy).
Kwa sasa anagombea Ubunge jimbo la Kisarawe
kupitia chama cha wananchi CUF akiwakilisha
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Kingwendu aliwaahidi wananchi wa KISARAWE kufanya kazi nayo vizuri na
kuleta maendeleo kabambe.Vilevile aliongeza kuwa hatoacha kufanya filamu
manake hicho Ni kipaji chake.
Comments
Post a Comment