DAZLAH'S PRIMARY SCHOOL HEADTEACHER REVEALS THE SECRET TO DAZLAH' DAZZLING PERFORMANCE!!! (jua siri)
Ni msanii anayetamba kwa sana na mwenye mvuto wa kimavazi, tabia ya kuheshimika, bidii na mkali jukwaani.Si mwingine bali Chile Monde aka Dazlah ama Suleiman ukipenda. Huku akizidi kujizolea wingi wa mashabiki kwa burudani la kukata na shoka na la kuridhisha, meza yetu ya habari iliamua kupeleleza zaidi siri ya mafanikio ya mfalme wa Kidekide. Tulifululiza moja kwa moja hadi shule ya msingi aliysomea Dazlah. Walimu kwa wanafunzi walitukaribisha kwa mbwembwe ndani ya shule ya msingi ya Timbwani Baptist iliyopo Likoni. Baada ya kujitambulisha na kusema tulilolitaka, mwalimu mkuu Bwana Elishama Obuhaka alikuwa mwenye furaha kwa kujivunia mwanafunzi wake kuwa superstar na kuwaikilisha shule yake. "Kusema kweli Suleiman alikuwa mwenye bidii na adabu sana.Darasani hadi uwanjani.Siri ya mafanikio yake Ni heshima kwa watu wote. Nakumbuka vyema Suleiman alikuwa Sanitary prefect kwa sababu ya usafi aliokuwa nao.Vilevile alikuwa mchezaji mpira hodari na tulimpenda sana.Twamtakia kila la kheri kwenye maisha yake ya muziki. Daima shule ya Timbwani baptist tutajivunia Suleiman."Alitudokezea mwalimu mkuu Obuhaka.
Namkubali sana mkali Dazlah
ReplyDelete