SIRI YAFICHUKA!!!!!!! MSANII WA KIKE SIS-P ATOBOA SIRI NA KUSEMA RABBIZLE ALIKUWA AKIMPIGA NA KUMDHULUMU KIMAPENZI!!!!


Lisemwalo lipo na kama halipo basi laja!Je,mwakumbuka wimbo "tabasamu"wa Sis-p? Kumbe hakukuwa na tabasamu lolote bali majonzi,mashaka na kilio.Sis-P,aliyekuwa amesajiliwa na produza Rabbizle na kutoa nyimbo kama TABASAMU na MSUPA alitoboa siri kuwa produza Rabbizle alikuwa akimpiga na kumnyanyasa kimapenzi.Akihojiwa kwa show ya Mashavmashav unirversity na presenta Gates Mgenge,dada huyu alifunguka wazi na kukubali kuwa Rabbizle alikuwa mpenzi wake.
Baada ya dhuluma hizo za kimapenzi,dada huyu aliamua kumpiga na chini Rabbizle na kufuata mkondo mwingine.Sis P alichukuliwa na produza Khalid wa A Million records (waeza muita Bonge la Bwana) na kutoa kibao kikali ambacho kwa maoni yetu twaweza sema ni disstrack kwa Rabbizle.Huku video hiyo ikiwa na wakwasi wa pwani kama Juma Shibe(MJ) na deejay Phauz,video hiyo imeanza kutawala kwenye stesheni tofauti za runinga.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA