KILA SIKU MWACHEZA WASANII WALEWALE.JE VIPAJI VIPYA VITACHIPUKA VIPI?- SWALI KWA MAPRESENTA!!!


Kila uchao talanta mpya zazidi chipuka na wasanii kujizatiti kufanya muziki mzuri.Ila cha kushangaza na kusikitisha ni kuwa kunao wasanii wenye vipaji ila nyimbo zinazosikika ni za wasanii walewale.Ndiposa crew kali ya muziki imeamua kuwacharaza viboko washika dau(pwani usanii pia tumepewa viboko vyetu) kwa wimbo wao mpya kwa jina "Twapambana".
Wasanii hao waliokuja pamoja chini ya Produza Shaa Sepeture wa 254 records iliyo maeneo ya Likoni ni Hardlizz,Kizaizai hapa na binti mkali anayechana kwa jina Myra.Watatu Hao waliamua kuja pamoja ili kuwasilisha wazo lao la kisanii kiujumla na kuwakilisha mawazo ya wasanii wenzao wanaochipuka.
"Wasanii hawa walikuja studio na kuniuliza maswali mengi kwanini presenters hucheza wasanii walewale kila siku na nikawaambia badala ya kuniuliza maswali watengeze kibao kipya kitakachozungumzia swala hilo,"alieleza Produza Shaa Sepeture wa 254 records.Kibao "twapambana" kitaachiliwa wiki hii ijumaa.Bila shaka tutahakikisha tunawapa link mpate kiskia.
Hivyo basi mwakubaliana na wasanii Hardlizz,Kizaizai na Lady Myra kuwa presenters hucheza wasanii walewale?

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA