KUMBE KUNA WASANII HAWAKULIPWA!!!!!!??????? SALAAALA!!!
Hivi majuzi wimbo ulikuwa "tukutane mombasa ohhh tukutane mombasa".Kisha tukakutana kweli Mombasa.Uga ukawa ni Mamangina,wasanii wakang'aa jukwaani.Sema Susumila huriraniiii samaki wakaingia,Nyota Ndogo kubebwa ili aonyeshwa penzi ili asiende,Dazlah yule yule wa ChileMonde classic (read Wasafi classic!) hadi vidolee aliwakamataa,Ally B na ziki lake la nazi,Sudi boy aliona bado,Wasiojali band (read Yamoto) waliojali sana mashabiki na wasanii 'wengineo.'
Basi ilikuwa kivumbi na moto jukwaani ila kumbe malalamishi na
manung'uniko yalikuwa yanatanda chini kwa chini.Hivi leo katika pitapita
zetu za kusikiza redio tuliskia live on air mtangazaji flani wa redio
akisema kuwa kuna wasanii hawakulipwa hata ndururu baada ya kutuimbuiza
katika tamasha hilo!!!!(sijui nicheke.....ama wacha tu).
Fununu ni kuwa wengi wa wasanii walilipwa pesa kidogo (elfu ishirini,wengine kumi,wengine tano na wengine yai).Mpaka dakika hii kuna wasanii wanalalamika kuwa hawajalipwa ila malalamishi yao yamevaliwa pamba maskioni na kuvaliwa miwani ya mbao.Jameni kukutana Mombasa tulikutana kweli hadi Alikiba mwenyewe alikutana na sisi (huyu alilipwa ama......????).Ni hayo tu na kama labda hukupata kakitu usijali tukutane Mombasa mwaka ujao.

Comments
Post a Comment