"MAJINI YAPO WASIKWAMBIE WENYE MAPETE" Kaa La Moto Kiumbe ATANGAZA MSIMAMO WAKE!!!!!!
Huku tetesi za ndumba,ushirikina na illuminati zikizidi kuwaka moto kwenye ulingo wa sanaa, Rapper Kaa La Moto Kiumbe ametoa mtazamo wake kuhusiana na mambo hayo. Rapper huyu aliye na wengi wa mashabiki ametuwacha midomo wazi kwani bado twashangaa jinsi gani anavyoamini ushirikina ilhali yeye ni mfuasi mkuu wa dini ya kiislamu. Cha kuchochea moto zaidi ni kuwa,La moto huonekana sana akivaa kanzu nyeupe na safi na kuonekana mcha Mungu ajabu.
La moto kwa wimbo mpya alioshirikishwa na rapper mwenzake Gaspery kwa jina NIAMBIE NIJUE amekubali kwa mistari kama "majini yapo wasikwambie wenye mapete" na mistari mingine zaidi.
Vile vile kuongezea msumari moto kwenye kidonda, Kaa la moto kiumbe amewadiss washikaji Fulani kimafumbo na kuwachapa kwa mistari hii......
"hapo wanajifunza kuruka mi nilizaliwa na mabawa..." Kwanini tutumie mate ilhali wino upo?
Jisikizie mwenyewe kwa kuupata wimbo hapa----->>>>> https://mkito.com/song/11114
Comments
Post a Comment