Wasojali Band Kufanya Collabo Na Yamoto Band
Ni vijana wanne ambao kwa sasa wanatesa sana na video ya wimbo wao wa NITALIA NAWE ambao walishirikiana na Kelechi Africana ambaye wamesajiliwa wote katika Kubwa Entertainment inayomilikiwa na Athman Babaz.
Katika siku za hivi karibuni, wamekua katika jiji la Nairobi kufanya media tour kuskuma video yao na mziki wao kwa ujumla. Na safari hio haikua bure kwani inaonekana imezaaa matunda hata zaidi ya waliyokua wanatarajia au wamepanga kutimiza.
Nasema hivyo kwa kua kwa sasa Wasojali Band wako katika hatua za mwisho
za mazungumzo ya kufanikisha collabo yao na Yamoto Band kutoka
Tanzania. Kupitia njia ya simu, nikiongea na meneja wao, Athman Babaz,
alieleza ya kwamba bado vitu kidogo tu wakamilishe ili makubaliano hayo
yaishe lakini kufikia sasa pale mazungumzo yalipofikia haoni kama kuna
kitu kitazuia collabo hio. Athman alizidi kueleza ya kwamba mazungumzo
yatakapo kamilika tu wataenda nchini Tanzania kwa madhumuni ya kurekodi
na kuandaa video ya collabo hio.
Hisani ya Mykol Baya Machampali
Hisani ya Mykol Baya Machampali
Comments
Post a Comment