KICHAPO BAADA YA KINGINE-DULLY MELODY ABWAGA DUDE!!!!!
Kila
uchao jamaa huyu kamwe hafumbi macho kwenye tasnia ya muziki hapa
pwani. Baada ya kutambulishwa rasmi na msanii wa dancehall
Fisherman, kinda huyu anamea mbawa na kuzidi kukita mizizi kwenye bahari
kuu ya muziki. Melody, aliyejimwaga uwanjani kwa mara ya kwanza kwa kibao
Hongera na kuwawacha mashabiki kwa kiu si haba. Amerudi tena kwa mara
nyingine kwa kibao chake kipya kwa jina YAGAYAGA. Huku akiwa chini ya
usimamizi wake producer NOOR MWAMBA, Dully amewatayarishia kibao hicho
kilicho na fleva tofauti na vile mlivyo mzoea. Hivyo basi, kibao YAGAYAGA
kitadondoshwa rasmi wiki inayofuata.
Comments
Post a Comment