POROJO ZA WIKI......KAZI NI KWAKO.NI SAWA SI SAWA????
Get link
Facebook
X
Pinterest
Email
Other Apps
Je ni
sawa kwa Msanii wa Kike kulala na Producer wake...? Au msanii kwa
msanii, au hata Presenter na msanii...??? Kwa sababu hawa wote ni work
mates...??
Ni msanii aliyekubalika na wengi na aliyevuma kwa vibao motomoto kama; mtoto wa shule,umaskini si kilema,kadem,toka nenda,kadem kameparara na nyinginezo. Msanii huyu aliyemaliza shule ya upili mwaka uliopita alifuzu na kuchaguliwa kwenye kikosi cha askari polisi kitengo cha AP. Ranny aliyekuwa studio ya Homeworks na kuhamia studio ya Mwamba records kwa sasa yupo kwenye kambi mafunzoni na aliahidi kuwa kamwe hatowacha muziki,atashughulika na muziki pamoja na kazi yake mpya ya kulinda usalama.
MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMANI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!! Huu bila shaka ni moto wa kuotea mbali na wasanii hawa wamejizatiti vilivyo kuwaleta warembo tele kwenye video yao.Sio warembo tu bali warembo wa kuvutia na kuridhisha nafsi. Wimbo wenyewe ni KARIBU MOMBASANI wa Benso,Kigoto na Miss Gee gee uliotoka mwisho wa mwaka Jana.Kamwe hatujui kulitumika mbinu gani kuwatafuta models wa sampuli hii ila tunachojua ni kuwa hawa sio wale wa kuokota mitaani au vichochoroni bali mabinti wanaofanya uanamitindo wa kulipwa. Bado tukiisubiri video yenyewe itakayotoka hivi karibuni,picha hizi dhahiri shahiri zadhihirisha uzuri unaokuja......
Mwanamuziki tokea pwani ya Kenya,P-day ametoa kauli yake kuhusiana na matukio ya mauaji ya wazee wanaoshukiwa kuwa wachawi pande za Kilifi. Msanii huyo aliyetamba kwa kibao tarumbeta,Nylon guitar,Visingizo,Niringe naye na vinginevyo amedokeza haya kupitia ukurasa wake wa facebook akikashifu vikali vitendo hivyo. P-day alisema ya kwamba usemi wake anaopenda kuusema kwa nyimbo zake....."MZEE HATEMEWI MATE" unapaswa kuwa kauli mbiu itakayochukuliwa na kuwekwa kama mtajo utakaowaokao wazee kutoka kwenye janga hili. Tukinukuu kutoka alichonakili kwenye akaunti yake ya facebook..... "Social cohesion department to buy the mzee hatemewi mate lebol ( uzee si uchawi ) nliamka tu nkatunga hii lebol din't know itafika huku ........Sasa vijana kilifi county walianza kuua wazee kwa kua niwachawi BT sio Kila mwenye mvi ni mchawi ..let's respect the old" JE MAONI YAKO NI YAPI KUHUSIANA NA PENDEKEZO LA P-DAY KUHUSIANA NA WAZEE KUUAWA?
Comments
Post a Comment