MUIGIZAJI MAARUFU WA PWANI Juma Shibe AMTEMBELEA MAMAKE MAREHEMU STEVEN KANUMBA.
Mwaka uliopita tulipata nafasi ya kuona na na muigizaji Juma Shibe ana kwa ana. Hapo basi mwandishi wetu hakulaza damu bali alimuhoji maswala kadha wa kadha na Shibe alifunguka kuwa, ndoto yake moja ni kumtembelea mzaziwe muigizaji marehemu Steven Kanumba wa Bongo. Shibe anayejulikana kwa jina lingine MJ alisifika kwa kipindi cha kusisimua Sumu kilichokuwa K24 TV. Jamaa huyu alizuru nchi jirani ya Tanzania akiwa pamoja na meneja wake Khalfan Julo.Wawili hao kando na kumtembelea mzaziwe Kanumba,walikua na mikutano na waigizaji tofauti wa Bongo na twashuku kumewekwa mikakati MJ kuingia kwenye ulingo wa movie za Bongo.
Usikae mbali,Pwani Usanii tutakujuza yatakayojiri.
Comments
Post a Comment