YOUNG NJITA AMSHIRIKISHA BEKA KWA WIMBO MPYA "SIWEZI JUTA."


Huku wengi wakimzoea kwenye mtindo wa kuchana hardcore hiphop. Gwiji wa chocolate city Malindi ameamua kububujika kiasi na kushika mkondo mwingine wa muziki. Japo bado Kanzu ni mpya sheikh ni yule yule kama wasemavyo waswahili, hivyo basi Njita amezuka akiangusha vina vikali kwa michano ya kimahaba. Huku akimshirikisha msanii wa kike Beka, video yao ina mvuto wa kipekee na uhalisia wa hali ya juu unaoleta dhana ya kimahaba. Wimbo wenyewe kwa jina SIWEZI JUTA upo chini ya uandalizi wa studio iliyosimama kidete kuleta talanta zinazoshika moto kwa kasi, Malindi Records. Bila shaka tusitumie mate ilhali wino upo....tazama uhondo wenyewe hapa----------->>>>>>>>>



Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA