MSANII CHANGEZ ALETA 'CHANGES' KWA JAMII.
Msanii Changez Ndzai kutoka hapa pwani, ambaye licha ya kujihusisha na sanaa yeye pia anajihusisha na maswala ya kuridisha kwa jamii kupitia Shirika lisilo kua la kiserikali. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Changez amekua akiwatia moyo ama ku inspire vijana wengi kwa juhudi anazopiga kila uchao. Hadi kufikia sasa Changez ambaye anazuru shule za Kaunti ya Makueni, amekonyezea picha hii kuonyesha jinsi anavyopenda kuwa karibu na watoto ambao ndio hunufaika kwa sana kupitia miradi wanayotoa kwenye shirika.
Comments
Post a Comment