MSANII ATIWA MBARONI KWA KUPACHIKA BINTI MIMBA!!!!!!
Msanii tajika anayetokea Malindi alijipata taabani jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa shtaka la kupachika binti ya watu uja uzito. Kiwanja, ambaye ni rapper tajika mkaazi wa Malindi alikumbwa na janga hili saa nne usiku pale familia ya binti huyo ilipojimwaya nyumbani kwake na polisi kibao. Kiwanja alibebwa hobela hobela hadi kituoni alipofungiwa na kuachiliwa asubuhi. Inakisiwa kuwa familia ya binti huyo ni wakwasi mno na hawakupendelea Kiwanja kuwa na binti yao.
Comments
Post a Comment