HIVI JE SUDI BOY ALIPIGANA NA MSANII CHIPUKIZI KOFFI?
Katika pitapita zetu mitandaoni,Tulikumbana na habari kuwa Sudiboy alishikana mashati na msanii wa Nairobi kwa jina Koffi.
Japo picha zenyewe zilidhihirisha Ni video,habari hizi zimeinua hisia za mashabiki zake na inakisiwa kuwa tukio hili huenda likiwa la kweli.kisa hiki kinafuatia baada ya Sudi kutojitokeza ili kumalizia video ya wimbo aliokuwa ameshirikishwa. Wimbo wenyewe ulikuwa wa msanii chipukizi Koffi aliyekuwa amemlipa Sudiboy hela kibao kama inavyosema blog huyo.
Juhudi zetu za kumfikia Sudi ziliambulia patupu ila tutawajuza pindi habari zikiwa full kipupwe!!!!Msikae mbali.
Comments
Post a Comment