BAADA YA KUBANDIKWA JINA LA "PRODUZA MPIGA BEAT ZA VIKEBE" TEE AZIDI KUNG'ARA!!!
Ni mtayarishi wa hits kibao tu, moja ikiwepo KideKide iliyompa Dazlah na Produza wake Tee sifa teletele. Produza Tee amekuza vipaji si haba na bila shaka ni mmoja wa maproduza tajika hapa Pwani. Hata baada ya msanii fulani kusema kuwa Produza huyu hajui lolote ila kupiga vikebe tu; Tee amewashangaza wengi kwani kwa sasa kibao alichokitayarisha kwa jina Iyo kinafanya vyema. Kibao hicho kilichowaleta wasanii Jay A na Dazlah pamoja kimepanda chati kwa wiki mbili tu baada ya kuachiwa. Hivyo basi wadau kaeni mkijua mdharau biu hubiuka!!!
Comments
Post a Comment