WASANII WAWILI WAPIGANIA KIKAO NA RAIS UHURU
Ilianza na nusu saa na rais na sasa ni Mr President. Tunawazungumzia wasanii Ordinary Bingwa na Sudi boy.Msanii wa hiphop OB alitoa wimbo NUSU SAA NA RAIS mwaka uliopita ndani ya Thundersound records na ukazua hisia kali kwa mashabiki na baadhi ya watangazaji wa radio. Juzi Sudiboy naye akatoa wimbo kwa jina Mr president chini ya Sq records na unafanya vyema tayari. Swali ni je kati ya hizi nyimbo mbili ni msanii yupi amepitisha ujumbe ambao kweli hata rais mwenyewe akisikiza atataka kukutana na msanii huyo? Na wimbo upi umepitisha ujumbe ipasavyo? Nusu saa na Rais ama Mr President?
Comments
Post a Comment