SINGA BABS AKIMSHIRIKISHA KENDI-TONITE
Huku sanaa ya pwani ikizidi kupata mpenyo kwenye soko la Nairobi msanii Babs hajawachwa nyuma.Gwiji huyu chini ya usimamizi wa Re-union entertainment na studio ya Mandugu dijital amebainitumebaini kuwa anao uwezo mkuu wa kuitikisa sanaa sio ya Kenya pekee bali Afrika Mashariki.Babs kwenye ujio wake mpya amemshirikisha binti shupavu mwenye umahiri kwenye tasnia ya muziki kwa jina Kendi.Wawili hawa walijitwika jukumu la uwapa burudani na kwa pamoja wakaandaa kibao kikali kwa jina #tonite. Unapousikiza wimbo huu hauta kuwa na budi kutikisa kichwa na kukubali utamu wake uliokolea kwani produza Scotch Fingaz aliamua kuunda mdundo wenye mvuto unaoziyeyusha hisia na kumpa msikilizaji nburudani tulivu la kukata na shoka.Basi ya nini tutumie mate ilhali wino upo? Tayari wimbo huu upo hewani kwenye vituo tofauti vya redio na umejaa mitandaoni.Utafute,usikilize burudani la kiuhakika.
Comments
Post a Comment