"SIJAFA BALI NI ACCOUNT YANGU ILIKUWA HACKED" FLIM-C AONGEA BAADA YA WATU KUDHANI AMEFARIKI.


Msanii Flim-C afufuka au tuseme hakuwa amekufa!Baada ya habari za msanii Flim-C eti amefariki,washika dau na mashabiki walianza kutuma jumbe zao za rambi rambi ila habari ni kuwa msanii huyu hajafa.Tuliwasiliana na msanii huyu na akatueleza kuwa sio yeye aliyeandika kuhusu mambo hayo bali ni mtu mwingine aliyehack account yake ya facebook na kuandika hivyo.Flim alitueleza kuwa hakuna vile anaweza kujichafulia hadhi na kutatiza familia yake kwa kusema eti amekufa.Mkali huyu wa kikosi cha Micharazo clique anayevuma kwa kibao 'tuje kule' alinena haya........
"Mimi sijafa na nipo salama salmini.Kuna jamaa amehack na kuingia kwa account yangu ya facebook.Nadhani alikua anataka kuniharia hadhi yangu.Hio picha ni yangu kweli ila sijafa.Nipo sana na nitazidi kuwapa burudani kemkem."
Habari ndiyo hiyo kwa waombolezaji.Futeni machozi.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA