MSANII WA HIPHOP HAPA PWANI ATEULIWA KUWANIA TUZO ZA MUZIKI NCHINI FRANCE!!
Yaonekana mwaka umemwanzia msanii Kiwanja anayetokea Malindi vizuri sana.Punde tu baada ya kutoa wimbo wake unaozungumzia maisha ya ghetto za Afrika, msanii huyu ameteuliwa kuwania tuzo za muziki za NRJ zinazofanyika nchini France kila mwaka. Wimbo wake Africano umeteuliwa kwa kitengo cha African influential song of the year huku akishindana na wakongwe wa muziki kutoka Ghana, Nigeria, Afrika kusini na Namibia. Kiwanja aliyesajiliwa ndani ya Malindi Records anatazamiwa kusafiri nchini France hivi karibuni kwa tamasha hilo. Twamtakia kila la kheri kwenye shindano hilo.
Comments
Post a Comment