JE NI KWELI NZUMARI AWARDS ZITAKUWA ZA GOSPEL PEKEE? N'GAMUA UKWELI HAPA!
Baada
ya tuzo za Nzumari zifanyikazo hapa pwani kupatwa na msukosuko na
kutofanyika kwa miaka miwili mtawalia, mashabiki na washika dau wa tasnia
ya muziki kanda ya Pwani walijiuliuza maswali mengi bila kupata
majibu. Hivi majuzi baada ya mwanzilishi wa tuzo hizo Eve Adhiambo
kuokoka na kumpokea Yesu kristo kama mwokozi wa maisha yake. Alikuja wazi
wakati alipokuwa anahojiwa ndani ya Baraka fm na Dj Lenium na kusema
kuwa tuzo za Nzumari zitafanyika ila wakati huu zitakuwa za
gospel. Sababu kuu ya tuzo hizi kugeuzwa kuwa za gospel, Eve alidai kuwa
ameamua kumtumikia Mungu na hii ndio njia moja ya kumtumukia. Binti huyu
vilevile alidai kuwa bado yupo kwenye biashara za kuandaa matamasha. Juzi
alikuwa na show moja ya kukata na shoka aliyomualika "malaika" si
kutoka mbinguni Bali Nairobi kwa jina Corazon Kwamboka. Cha msingi ni kuwa kuna uwezekano mkubwa tuzo hizi za Nzumari gospel Awards kufanyika
mwezi Aprili ndivyo alivyomalizia mwanadada Eve.
Comments
Post a Comment