DADDY SELLE,ALKENIA LUV..wazua vijimambo mambo visivyoeleweka! Soma upate uhondo!
Nakumbuka vizuri sana mwezi February mwaka huu msanii Daddy Selle alitangaza wazi kuwa amewacha muziki kabisa na ameamua kuwa mcha Mungu, msanii huyo aliyekuwa kwenye kikosi cha studio ya Mwamba records alisema kuwa amewacha mambo ya ulimwengu na anafuata kanuni na sheria za uislamu daima dawamu. Vilevile tusimsahau msanii Alkenia Luv, msanii gwiji wa RnB hapa pwani. Alkenia Luv miezi michache iliyopita aliokoka na kuahidi kuimba muziki wa injili. Jambo la kushangaza ni kuwa yuyu huyu Daddy Selle aliyedai kuwacha muziki na kumtukuza Mungu leo hii ameachia kibao kipya kwa jina NITAMUOA.Maajabu hayaishi. Mwenzake Alkenia Luv hana haya hadi leo hajawahi rekodi hata wimbo mmoja wa injili. Cha kushangaza wanaendelea kuwasifu mabinti na mapambo tu, Mungu kando!!!