SIRI YA MSANII HUYU KUANDAA VIDEO YAKE NDANI YA NYUMBA YA TYCOON FLANI WA KENYA YAFICHUKA!!!!


SIRI YA MSANII HUYU KUANDAA VIDEO YAKE NDANI YA NYUMBA YA TYCOON FLANI WA KENYA YAFICHUKA!!!!

Pilka pilka zikizidi pamba moto kisiasa, wasanii wa Kenya wameamua kutosubiri moto huu kuzima.
Jambo hili ndilo lililomfanya msanii anayeibukia vizuri kutoka Kenya, Beka the Boy kuingia ndani ya nyumba ya mchoraji sifika duniani Giampaolo Tommasi ili aweze kutengeneza video yake.
Hivi je kusudio lake kuu lilikua lipi? Meza yetu ya habari ilibaini kuwa msanii huyu alitaka kupata picha na mvuto wa tamaduni tatu tofauti zikiwemo Swahili, Giriama na Italiano. Nyumba ya jamaa huyo, Giampaolo Tommasi imepambwa kwa picha za kuvutia zinazoleta tamaduni zote tatu pamoja hivyo basi mshikamano na maana fiche zimebebwa vyema kabisa kwenye mandhari haya.

Je video ya wimbo wenyewe ni ipi? Ni swali wanalojiuliza wengi wa mashabiki. Tukizipunguza dukuduku zenu, wimbo wenyewe wajulikana kama "Jidai" uliotayarishwa na produza Totti La Inter na video imetayarishwa na produza anayebobea sana kwa jina Marvin Brudaz wa Undepicted Films and photography.
Uzinduzi wa video utafanyika Malindi Fermento 9 September 2017 kuanzia 11:00 usiku. Tazameni picha kisha mtapata yaliyojiri....


Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA