DOGO RICHIE ANIHARIBIA BIASHARA KWA KUTONGOZA WASANII WA KIKE WAKIJA STUDIO--PRODUZA AMZ ATOBOA SIRI!
DOGO RICHIE ANIHARIBIA BIASHARA KWA KUTONGOZA WASANII WA KIKE WAKIJA STUDIO--PRODUZA AMZ ATOBOA SIRI!!!
Idadi ya wasanii wa kike ndani ya studio za Tempoz imepungua sana jambo lililomfanya Produza Ammz kuongea.
Jambo hili limeleta ugonganishi kati ya studio ya Tempoz na msanii Dogo Richie kwani yasemekana kuwa msanii huyu ana tabia ya kuwatongoza wasanii wa kike pindi wanapokuja studio. Dogo Richie kwa sasa, kama tulivyobaini ametongoza zaidi ya wasanii sita wa kike na kuwadanganya kuwa atapiga nao kolabo na kuwashika mkono kimuziki ili waweze kujulikana kwa urahisi. Jambo hili ndilo lililomkera produza Amz ambaye vilevile ni mmiliki wa studio hiyo. Amz alisema ya kuwa jambo kama hilo linamuharibia biashara na hadhi yake kama produza.
"Wasanii wote wa kike wameacha kuja studio na pia idadi ya customers wangu wa kike pia imepungua tangu Dogo Richie akinyage studio. Tabia kama hizi ndogo ndogo ndizo zinazokandamiza sanaa ya Pwani na kupoteza vipaji vya mabinti bure. Nimejaribu kuongea na Dogo Richie na twasuluhisha jambo hili japo wasanii hao wa kike bado hawajarudi. "Alieleza Amz.
Juhudi zetu za kumfikia Dogo Richie kuhusiana na tetesi hizi hazikufua dafu. Sasa haya nayo ndio majanga.
Comments
Post a Comment