KILA MTU NA MSIMAMO WAKE NDIO SANAA INAVYOENDA ASEMA PRODUZA AMMZ

Produza na mmiliki wa studio za Tempoz, produza Ammz Jadidi au Tone la Maji ametoa kauli yake kuhusiana na maoni yatolewayo kuhusu sanaa.
Haya yote yanajiri baada ya maswala kadha wa kadha kuibuka, yakiwemo show ya msanii Tekno Miles iliyobuma na Anita Santuri wa Pwani Celebrity Awards kusuta Cartels za muziki wa Pwani. Ammz amekuwa muwazi sana na kusema kuwa kila mmoja huwa na msimamo wake dhabiti anaouamini.
Pasi kupoteza muda Soma alichonakili produza huyo hapa....
"Nimekuja kugundua hapa Kenya usiwahi kubishana na mwenzako kuhusu sanaa ya mziki inavyopaswa kuendeshwa. Kwa sababu kila mtu anajua na anaamini kila "point" anayoitoa. Washikadau wako na misimamo mikali wanayoiamini pa kubwa sana. Tatizo ni kuwa misimamo hii inatofautiana kutoka kwa mshikadau mmoja hadi mwengine. Na endapo utalazimisha kubadili msimamo wa mtu basi huenda ukajijengea chuki na huenda ukaharibu hata kazi yako. Hali hii imefanya wale walio wanyonge kwenye safari kubaki kenyenyekea na kujifanya kana kwamba kila kitu kiko shuari lakini mwisho wake inatokea kuwa wanakuwa kama watumwa katika kazi zao. UNAFIKI WA MAWAZO."

Comments
Post a Comment