"MAHABUBA" MSWAZZY MASAUTI TAYARI KUACHIA WIMBO MPYA KWA MTINDO MPYA!!!!
Meli ya pwani imekita nanga na ya mgambo ikilia bila shaka kuna jambo. Alitamba kwa vibao kama uko mbali, Siwezi, Niko nawe na vinginevyo na ndiposa gwiji wa ukuzaji talanta Ted Josiah akamchukua kumtambulisha kwenye sauti mpya SWARNB. Masauti tayari ashatayarisha kibao kipya kwa jina Mahabuba kilichokolea wingi wa tanakali za uswazi na mvuto wa ndimi za asili ya kipwani. Huku tarehe ikiwa imepangwa 27 mwezi huu, kikosi cha SWARNB records kikiongozwa na Ted Josiah kwa Mara ya kwanza kitatambulisha kazi mpya ya Mswazi Masauti na Mashabiki lazima watakubali matokeo kwani palipo na wazee bila shaka hapakoseki jambo. Kwa hiyo, kaeni mkao wa kula Masauti anawaandalia Mahabuba.
Comments
Post a Comment