DIAMOND ASEMA HASHIKI SIMU YA ZARI KWA SABABU HATAKI KUUMIA MOYO.
Daah hii sasa balaa tupu,ingawa wana mtoto masuperstar hawa wawili bado wana matatizo ya uaminifu. Diamond president wa Wasafi amemwaga mtama kwenye kuku wengi na kudokeza hadharani kuwa hawezi kamwe kushika simu ya mkewe Zari kwa sababu hataki kuumia moyo.
Swali ni je wewe waweza shika simu ya mumeo ama mkeo?
“Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa,” alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari.
Diamond aliendelea kutoa sababu za kutoshika simu yake, “sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye (Zari) ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi sometimes anaweza akamjibu mtu akaitikia tu poa, kwangu mimi kikanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo ikaniumiza, kwahiyo sitaki kabisa kushika simu yake.”
Pamoja na kwamba yeye hashiki simu ya mpenzi wake, vipi kuhusu Zari kushika simu yake?
“ Simu yangu mi haina password naiachaga tu lakini nafikiri na yeye ni mtu wa dizain hizo ambaye hataki kabisa kudiriki kushika simu yangu, yaani simu zinaleta ugombanishi sana.”
Diamond pia aliwashauri watu wengine kutoshika simu za wapenzi wao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika.
“Kwahiyo simshauri mtu kushika simu ya mpenzi wake, cha muhimu tu kuzingatia kama anakupenda anakujali anakuheshimu na umuone na hivyo vitu, lakini kwenye simu yake mwache afanye chochote anachojua yeye.” Alisema Diamond.
-Millardayo
Comments
Post a Comment