MIMI HUSAIDIA NINAPOWEZA-NYOTA NDOGO AONGEA BAADA YA CHIPUKO LA CONJESTINA.
Baada ya kuachia video YouTube ya kuhusiana na wasia wake kwa bondia wa kike Conjestina Achieng, mama mlezi wa sanaa ya pwani Nyota Ndogo amekuja wazi na kuongea kuhusu misaada yake. Japo kidogo Nyota alisema kuwa yeye hutumia ufanisi wake kimuziki kusaidia yatima........
"WATU WALIOULIZA YEYE NYOTA KAFANYA NINI KWAO MOMBASA NDIO AMTETE CONJE? Wengi wanafikiria kusaidia nikutoa mamilioni ya hela kutoka mfukoni mwako. Sina uwezo huo but kile kidogo uwa ninacho mimi ushea. NATUMAI MPO SALAMA. kwanza kabisa kwetu Mombasa nimejiusisha na mambo mangi na kujituma. Sijui kama unajua huwa nashughulikiwa watoto yatima kutoka nyumba tafauti mombasa hadi voi. Utoa nguo zangu mwenyewe ama za watoto wangu ama naomba watu fb kuchangia kutuma nguo ili zipewe watoto hao. Nafikiria kwa watu wamombasa wanaonifatilia vizuri wanajua. Nimetoka kwa maisha ya shida nikiwa mdogo hivyo unikumbusha mbali napoona watu wakipata tabu. kila skuku ya idd mimi ula na mayatima nitaitisha mchango fb wasipotoa nitajikaza nitawalisha mwenyewe. nimeshawai kuchanga pesa fb nikafikisha elfu 60 nikanunua chakula nikalisha nyumba sita za watoto mayatima. Nasaidiwa sana na watu wa fb kusaidia watoto hawa. Nimeshawai kununua vitabu vya shule kwa watoto na pesa yangu mwenyewe. kwaivyo navyosema haya fb nikuwa najua watu wa fb usaidia na wanaonifatilia wanajua uwa naomba misaada kuwasaidia watoto wale na wakifurai sio mimi nimewafuraisha uwa ni mimi na marafiki zangu wa fb.sijui kama nimekuridhisha.
SIJITANGAZI KWAKUWA HUWA SISAIDII PEKE YANGU NAONYESHA TU KUWA PAKIWA NA SHIDA MAHALI SIONI HAYA KUOMBA MSAADA FB NA WATU HUTOA"
Maneno ya Nyota Ndogo.
Comments
Post a Comment