KHALFAN JULO MENEJA WA MJ ASEMA MENGI YANAPASWA KUFANYWA KWA BURUDANI LA PWANI.
Baada ya ushindi wa Juma Shibe almaarufu MJ, meneja wake Khalfan Julo amepasua mbarika kuhusiana na tasnia ya burudani la pwani. Khalfan,ambaye vilevile ni muigizaji mkali na assistant director wa Coast Films alidokeza haya huku akimtayarisha Mj kwa ziara ya kuzuru Tanzania. Julo alidokeza kuwa pwani ina vipaji vingi na wakati umefika vipaji viweze kupepea.
"Sio uimbaji au uigizaji,pwani imejaa vipaji tele na viongozi wa serikali wanapaswa kutilia mkazo kwenye ukuzaji talanta. Hii itasaidia sana vijana kujiajiri na kupigana na madawa ya kulevya."Alisema Julo.
Comments
Post a Comment