CHIKUZEE NA SUSUMILA BIFU YAZIDI KUNOGA!!!


“Kama Susumila ana kichwa kigumu mimi nimeharibika na kama ananilenga mimi basi amelenga pakavu,kwanza Susu hawezi kuimba yeye afanye rap wala sikuimba mana kuimba hawezi na sisi ndio tulimfundisha Susu kuimba kwa hivyo asijiite sijui rais wa wanamziki wa pwani'’. Haya si maneno ya mwengine bali ya msanii Abdalla Chikuku almaarufu Chikuzee wakati akihojiwa na kituo cha pilipili fm.
Chikuzee ambaye alishawahi kufanya collabo na Susumila kwenye nyimbo mbili za Hidaya pamoja na Ngoma Itambae ambazo zilitamba kwenye soko la mziki wa Kenya, alimtaja msanii Susumila kama msaliti mkubwa.
“Susumila ni msaliti na tulivyo kubaliana sivyo alivyo fanya na anapenda kudandia wasanii wengine ili azibe aibu yake yakutojua kuimba na kama ni star kweli atoe ngoma peke yake na ifanye vizuri hapo ndio nitamheshimu lakini kama mwendo ni huo wakudandia namwona mtu wakawaida tu,” alisema Chikuzee.

Chikuzee kwa sasa anatamba kwa ngoma yake mpya kwa jina Simuachi iliyotengenezwa Number one Records chini ya mko wa producer mkali TK2.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA