Mziki wangu wazidi kung'ara baada ya Grandpa Records, Asema Kidis
Msanii Kidis aliyevuma kwa kibao chake Kamua leo, amekiri kuwa taaluma yake ya kimziki imekuwa nzuri zaidi baada ya kuachana na Grandpa Records. Msanii huyu ambaye ametoa kibao chake kipya Viroboto kinacho zidikuchezwa kwenye stesheni mbalimbali, anasemekana kuzozana na CEO wa Grandpa Records Refigah, alisema kuwa career yake inazidi kuwa better baaada ya kuachana na Grandpa ambayo alisema hakufikia targets zake alipokuwa pale. Hata hivyo Msanii Kidis aliongezea kuwa mziki umekuwa mgumu sana kwani hata maDJs, maproducer na hata mapresenter siku hizi wanaimba. Aliongeza kusema sasa yuko free kufanya mziki wake katika production yoyote.
BY Nina Kagia
Comments
Post a Comment