FIDEMPA BILA SHAKA AMEIPEPERUSHA BENDERA YA DANCEHALL PWANI JUU KABISA
Alitoka Pwani akiwa kinda kwa ulingo wa muziki na kuelekea Uganda kubahatisha bahati yake.Huku nyuma kila shabiki aliwachwa roho juu na kumtakia kila la kheri kwa njia aliyoichukua.Haikumakiza hata mwaka msanii wa ragga na dancehall Phidempa alipovunja ufuo na kutiririsha vibao vikali na vya kusisimua na kuchukua nafasi kula mkeka mmoja na wakali wa Afrika mashariki.Hivi majuzi bingwa huyu ambaye mizizi yake ya muziki iliota hapa Pwani alitoa kibao akishirikiana na Proff na kikafanya vyema sana.Hivi saa video yake DANGEROUS inachafua charti za muziki wa Afrika mashariki.