MWINYI KAZUNGU (TOP MASHARIKI) AMSIFIA DULLY MELODY KWENYE INTERVIEW MPYA!!!


MWINYI KAZUNGU (TOP MASHARIKI) AMSIFIA DULLY MELODY KWENYE INTERVIEW MPYA!!!

Mtangazaji sifika Afrika Mashariki, Mwinyi 'Mtetezi' Kazungu wikendi iliyopita alidunda Pwani kwa kuandaa show kadhaa za kipindi chake cha Top Mashariki TV show kwa KBC.
Mtetezi, katika pilka pilka zake alipata fursa ya kumhoji msanii Dully Melody katika maeneo ya Pirates beach na hapo ndipo aliposhuhudia kipaji cha mkali huyu kutoka Pwani.

"Kusema kweli, Dully Melody ni mwenye kipaji si haba.Ni mara yangu ya kwanza kumfanyia interview na nimeona kipaji chake kitanawiri na mimi binafsi pia nitahakikisha dau Lake la sanaa laelea Juu. Nimekuza vipaji vingi vya Pwani na Dully bila shaka amenionyesha anao uwezo."Alidokeza Mtetezi.

Presenta huyu ambaye yupo mstari wa mbele kwa kuenua vipaji vipya si Pwani pekee bali Kenya nzima aliongeza kwamba atarudi Pwani kuja kufanya show zaidi za kipindi chake cha Top Mashariki kwani huku ndiko kwenye chimbuko halisi la vipaji vinavyoibukia. Kwa mengi zaidi msikose kuitazama show kubwa Top Mashariki ijumaa hii saa nne usiku kwenye runinga ya KBC.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA