MSANII MKUBWA WA PWANI AGEUKA KUWA MGANGA HATARI!!!!!!
Ni habari motomoto na za kutamausha zilizofikia meza yetu ya habari hivi majuzi. Msanii chipukizi anayetokea mtaa wa Mbandi,gatuzi dogo la Kinango amewashangaza wengi pale alipoupiga teke usanii wake kwa muda na kujiunga na uganga.
Msanii huyo chipikuzi anayejulikana na wengi kama Boss Michapo amekua mganga sifika guku akivutia wateja wengi kutoka kanda yote ya pwani. Michapo amekua akivuma kwa vibao motomoto vinavyopigwa sana kwenye madisko vumbi na disko matanga.
Ilifikia wakati msanii huyo alipogonjeka na kwenda nchi jirani ya Tanzania kutibiwa ndipo aliporudi na kuwa mganga hodari. Inakisiwa kuwa Boss Michapo alienda Bongo na kununua mkoba wa uganga. Hivi sasa msanii huyu huenda studio na kulipia wasanii wenzake wamuandikie nyimbo kwa sababu hana muda wa kukaa chini na kuandika nyimbo. Jamaa huyu vilevile amesema hivi karibuni atasifika Afrika Mashariki yote kwa kuwa amepanga vibao motomoto na atatumia nguvu zake za kiganga kupenya kwenye soko la muziki. Vilevile amewakaribishwa wasanii wanaotaka kuvuma kumtafuta ili awasafishie nyota zao za kisanii.
Comments
Post a Comment