Posts

Showing posts from April, 2016

TABIA YA KUCHUNGULIANA NYETI YASHUHUDIWA WAKATI WA VIDEO YA 'GOODMORNING' YA MSANII BABU DEE MAPETE!!!!

Image
Sijui huwa swaga ama ndio style za wasanii wakati wanatumbuiza. Jana kwenye club ya Valencia inn, msanii Babu dee Mapete aliyekuwa yuatambulisha video ya wimbo wake wa 'good morning' alifanya masihara ya kushangaza kama muyaonayo kwenye picha. Tabia hii ya kudon'goa na kuchunguliwa hupendwa sana na wasanii ila tukiweka hayo kando...jitazamie video ya 'goodmorning' kwenye mtandao wa YouTube na hivi karibuni mtaipata kwenye runinga zenu.

Nyakua nakala yako ya PEOPLE DAILY ‪#‎tribe43‬ ndio kusema.

Image
TOKA JIKONI

Hustlajay Maumau APATA BEMBELEZI ZA Nyota Ndogo !!!!!!!!

Image
Jamaa wa hiphop damu ameamua kulainika na kutapika mahaba. Hustla Jay tuliyemsikia kwa mara ya kwanza kwa kibao chake kikali "minyororo ya haki" ameamua kulainika na kujiunga na kundi la wabana pua. Jamaa huyo ameshirikiana na Nyota Ndogo kwenye ujio wake mpya unaoleta dhana ya mahaba motomoto. Kaa mkao wa kula kwani ngoma hio haipo mbali kuwachiliwa.

MUIGIZAJI MAARUFU WA PWANI Juma Shibe AMTEMBELEA MAMAKE MAREHEMU STEVEN KANUMBA.

Image
Mwaka uliopita tulipata nafasi ya kuona na na muigizaji Juma Shibe ana kwa ana. Hapo basi mwandishi wetu hakulaza damu bali alimuhoji maswala kadha wa kadha na Shibe alifunguka kuwa, ndoto yake moja ni kumtembelea mzaziwe muigizaji marehemu Steven Kanumba wa Bongo. Shibe anayejulikana kwa jina lingine MJ alisifika kwa kipindi cha kusisimua Sumu kilichokuwa K24 TV. Jamaa huyu alizuru nchi jirani ya Tanzania akiwa pamoja na meneja wake Khalfan Julo.Wawili hao kando na kumtembelea mzaziwe Kanumba,walikua na mikutano na waigizaji tofauti wa Bongo na twashuku kumewekwa mikakati MJ kuingia kwenye ulingo wa movie za Bongo. Usikae mbali, Pwani Usanii tutakujuza yatakayojiri.

KINGMONDE AKA DAZLAH KIDUCHE AWACHIA KICHUPA KIPYA!!!!

Image
Baada ya kutoa vibao motomoto hivi majuzi kama Bangereba, Kidekide, Cheza Kidogo na Iyo, Dazlah Kiduche ukipenda Chilemonde ameachia video mpya. Wimbo huo kwa jina Nitalia umeandaliwa na Produza Tee ambaye amemshikilia Dazlah tangu kinda. Msanii huyu vilevile amekuwa kwenye tour za nchi za nje kama vile Madagascar na Dubai. Hivyo basi tusitumie mate ilhali wino upo, jitazamie mwenyewe video hiyo iliyoandaliwa na PichaMoja production. Tukitumia maneno ya Dazlah mwenyewe, hii hapa video----------------- -Nitalia Video is Now Out!!! Wapenzi wa Muziki wangu Click the link... Watch, Comment and Share the Link All over The world.. Please need your Support Please... I love you All >>>>>>>>>>>>>>>>>>> https://youtu.be/MTpV5yLIXVQ

LIL GUY G USITUDANGANYE!!! AKOTHEE NI WHACK ARTISTE- RAPPER KASSAMONEY AFOKA!!!!

Image
Ajulikana kama Kassamoney Brian rapper anayependa kuweka ukweli wake hadharani bila uoga. Jamaa huyu ambaye ni mkuu wa kikosi cha Coastside militia alimuingilia video producer LilGuy G alipodai kuwa Akothee huenda akawa best female African artiste. Tukinukuu maneno aliyopachika kwenye account yake ya facebook. "Lil Guy G' Ukisema Akothee Might be the best Female Artist in Africa cuz of the hardw ork she puts in her music then you have to know You are simply saying Papa Dennis Might be the Best Male Gospel Artist In Africa .. -Hard Whack indeed" Hivi mwakubaliana naye kweli????

TAZAMA TAMASHA YA PWEZA PARTY ILIVYOFANA.MLO KWA WINGI.(PICHA)

Image

Wasojali Band Kufanya Collabo Na Yamoto Band

Image
Ni vijana wanne ambao kwa sasa wanatesa sana na video ya wimbo wao wa NITALIA NAWE ambao walishirikiana na Kelechi Africana ambaye wamesajiliwa wote katika Kubwa Entertainment inayomilikiwa na Athman Babaz. Katika siku za hivi karibuni, wamekua katika jiji la Nairobi kufanya media tour kuskuma video yao na mziki wao kwa ujumla. Na safari hio haikua bure kwani inaonekana imezaaa matunda hata zaidi ya waliyokua wanatarajia au wamepa nga kutimiza. Nasema hivyo kwa kua kwa sasa Wasojali Band wako katika hatua za mwisho za mazungumzo ya kufanikisha collabo yao na Yamoto Band kutoka Tanzania. Kupitia njia ya simu, nikiongea na meneja wao, Athman Babaz, alieleza ya kwamba bado vitu kidogo tu wakamilishe ili makubaliano hayo yaishe lakini kufikia sasa pale mazungumzo yalipofikia haoni kama kuna kitu kitazuia collabo hio. Athman alizidi kueleza ya kwamba mazungumzo yatakapo kamilika tu wataenda nchini Tanzania kwa madhumuni ya kurekodi na kuandaa video ya collabo hio. ...

GWIJI WA SPOKEN WORD NA POETRY CHANGEZ NDZAI AZIDISHA UHUSIANO WAKE NA WASHAIRI WENZAKE.

Image
Msanii Changez Ndzai azidisha uhusiano wake na malenga wenzake (POETS)wa nchi za ulaya, leo hii ameandika shairi la kumtakia heri njema ya siku ya kuzaliwa malenga maarufu nchini marekani Blaq Ice . HAPPY BIRTHDAY KING OF POETRY! Hello my big bro back in Chicago soil, Blaq Ice the one and only king of art, Long live to see your great grandchildren oil, Let the clouds form your names part. Let you enjoy this day with happy mail, Row row your best of life's swift boat, May you live to be the head no not tail, Roast the meat from the fat goat. Happy birthday as you blow candle's rail, My sincere greetings from Kenya let it float, Enjoy this day in slow motion as a snail, For happiness is friends surrounding your lot. Live long the king of American poetry nail, You are hitting another year ahead in retreat, Wishing you all the best endeavor in life's dial, Salute! Bro, celebrations on Chicago's street...Wow-wow...CHANGEZ!

Eddy Ticha ATAMBULISHA VIDEO YAKE MPYA.

Image
Alikua kwa kikosi cha wasanii kwa jina Watash. Si mwingine bali Eddy Ticha. Jamaa huyu kwa sasa ameachia video yake mpya inayojulikana kama Zawadi. Wimbo huo ulitayarishwa na Morbiz Sheriff wa Thundersound records na video iliandaliwa na Link junior. Itazame kwa mara ya kwanza hapa------>>>>> https://youtu.be/uno9Q2OnDuI

SOURCE LYRICS BY DULLY MELODY

Image
CHORUS oooh my babiee eeeeeeaaah,your the source of my of my success. oooh my babiee eeeah your the source of my happiness. unipende mimi usipende waleeee unipende mimi mamaaa×2 VERSE 1 uzuri wako ndo unanifanya mimi nijidaiii,hata wapambe wanatamani melody i gonna dieee.."nipo safarini subiria natafuta vumilia×2 oooh nikikosa kazini hata njiani napata,hata nikifumba macho nikipapasa napata×2,I give u love,you give me love my babiee oooh hooa×2,yu give me love i give u love my babiie ooowaa,yu give love i give love my wife to be maamaaaa×2 CHORUS Ooh my babiee eeah your the source of my success,ooh my babie eeeah your the source of my happiness,unipende mimi usipende waleeh,unipende mimi mamaa×2 VERSE 2 unanijaliii ninakujali mamaaa,"kwa kila hali ntakutunza nanitakupenda saanaa,kwa kila hali ntakutunza mamaa nanitakupenda saanaaa. nilipokosa ngarawa ulinipenda mamaa,sasa narudi na dawa utaridhika babiee×2. CHORUS ooh my babiee eeaah your ...

PWANI USANII BLOG 001

Image
Pwani Usanii twawakilisha pwani kwa habari za wasanii moto moto

"MAJINI YAPO WASIKWAMBIE WENYE MAPETE" Kaa La Moto Kiumbe ATANGAZA MSIMAMO WAKE!!!!!!

Image
Huku tetesi za ndumba,ushirikina na illuminati zikizidi kuwaka moto kwenye ulingo wa sanaa, Rapper Kaa La Moto Kiumbe ametoa mtazamo wake kuhusiana na mambo hayo. Rapper huyu aliye na wengi wa mashabiki ametuwacha midomo wazi kwani bado twashangaa jinsi gani anavyoamini ushirikina ilhali yeye ni mfuasi mkuu wa dini ya kiislamu. Cha kuchochea moto zaidi ni kuwa,La moto huonekana sana akivaa kanz u nyeupe na safi na kuonekana mcha Mungu ajabu.  La moto kwa wimbo mpya alioshirikishwa na rapper mwenzake Gaspery kwa jina NIAMBIE NIJUE amekubali kwa mistari kama "majini yapo wasikwambie wenye mapete" na mistari mingine zaidi. Vile vile kuongezea msumari moto kwenye kidonda, Kaa la moto kiumbe amewadiss washikaji Fulani kimafumbo na kuwachapa kwa mistari hii...... "hapo wanajifunza kuruka mi nilizaliwa na mabawa..." Kwanini tutumie mate ilhali wino upo?   Jisikizie mwenyewe kwa kuupata wimbo hapa----->>>>> https://mkito.com/song...

Kigoto Mmbonde VS Mswazi Masauti Kenyanboy!!!!!!!! HIVI JE HAWA JAMAA WAWILI WAKIPIGA COLLABO NANI ATAMFUNIKA MWENZAKE???????

Image

CELEBRITY PHOTO OF THE DAY:

Image
NAME: Philo Bliver (Philip Zuma) Radio presenter Sheki FM. Kipindi cha BEMBEA LA WATOTO every Saturday morning. Nurturing young talents,poetry,spoken word and music.

WATALII MUSIC FAMILY: MALINDI LAZIMA KIELEWEKE!!!!

Image
Huku Chocolate City Malindi wakizidi kujigamba kwa ukwasi wa hiphop, kikosi cha Watalii Music Family kikiongozwa na Makushabu kimejipa jukumu la kuupeleka muziki wa Malindi ulimwengu mzima. Tetesi zinazojiri ni kuwa kikosi hiki kimeungana na kundi moja la wasanii wa Nairobi wanaojulikana kama Maafleva Music.  Hivyo basi, kipenga cha sanaa tayari kishapulizwa na Watalii Music ishang'oa nanga.

VIDEO YA MNS-BAIYOYO TAYARI!!!!

Image
Baada ya mashabiki wa MNS wa Kikosi cha muziki cha HalfBouncy, kusubiria video ya Baiyoyo kwa zaidi ya miaka miwili. Hatimaye subiri yao imevuta kheri. Msanii huyu ambaye kwa sasa yupo uarabuni kwa minajili ya pesa tayari alishatayarisha video hiyo na ataiwachia wakati wowote dakika hii. Wimbo Baiyoyo alimshirikisha Susumila ila kwa ajili ya umbali wa kusafiri ikambidi aandae video hiyo peke yake.

POROJO ZA WIKI......KAZI NI KWAKO.NI SAWA SI SAWA????

Image
Je ni sawa kwa Msanii wa Kike kulala na Producer wake...? Au msanii kwa msanii, au hata Presenter na msanii...??? Kwa sababu hawa wote ni work mates...??

HEKO KWA AUDIO\VIDEO PRODUCER MSANII WIZZOH CLASSIC WA WIZZOH EMPIRE KWA KUPATA MTOTO!!!!!!TUKUITE BABAKE NANI VILE?

Image

NYOTA NDOGO AKARIBISHWA KWA SHANGWE NA MBWEMBWE NA WASHIKA DAU WA SANAA YA PWANI. (Tazama Picha)

Image
Baada ya kuzuru Denmark kwa show za muziki, mama wa sanaa ya pwani Nyota Ndogo alikaribishwa kwa mbwembwe kibao na shangwe nyingi alipotua tu kutoka Denmark. Tamasha hilo dogo lilifanyika mkahawa wa Dan's Lounge na washika dau wa sanaa kama DJ Elon, Gates, Susumila, Hassan Feisal, Producer Khalid na wengineo walifika kumlaki Nyota. "Thanks kwa kila mtu aliejitokeza kwenye show hii ilioandaliwa kwaajili ya makaribisho ya nyumbani.@hassan falsal mufti @ Hawkings Kidiavai Pday Hurrikane Kenya Sis P Queen susumila yusuf @jay crack @priducer khalid yani nikisema nitawaja wote sitamaliza.ila shukran sana yani sikuamini kabisa kulivyo jaa wasanii wote muliokuja tupo pamoja.@Eric mmu ahsante kwa maandalizi haya". Alisema Nyota. Tazama picha

KIKOSI CHA NUMBER-ONE RECORDS KAMWE HAKILEGEZI KAMBA.

Image
Huu hapa ujio mpya unabisha hodi kwenye jukwaa la sanaa ya Pwani. Kigoto Mbonde akiwa sako kwa bako na Iddi Singer. Mkono ni ule ule wa gwiji wa kazi zake TKMBILI. Kaeni mkao wa kula,haribika kabisaaaa!!!!

KICHAPO BAADA YA KINGINE-DULLY MELODY ABWAGA DUDE!!!!!

Image
Kila uchao jamaa huyu kamwe hafumbi macho kwenye tasnia ya muziki hapa pwani. Baada ya kutambulishwa rasmi na msanii wa dancehall Fisherman, kinda huyu anamea mbawa na kuzidi kukita mizizi kwenye bahari kuu ya muziki. Melody, aliyejimwaga uwanjani kwa mara ya kwanza kwa kibao Hongera na kuwawacha mashabiki kwa kiu si haba. Amerudi tena kwa mara nyingine kwa kibao chake kipya kwa jina YAGAYAGA. Huku akiwa chini ya usimamizi wake producer NOOR MWAMBA, Dully amewatayarishia kibao hicho kilicho na fleva tofauti na vile mlivyo mzoea. Hivyo basi, kibao YAGAYAGA kitadondoshwa rasmi wiki inayofuata.

Mishe Mshe! JE TAMASHANI NI WAPI?? GATES NA DEEJAY ELONN WAWAITA !!!

Image
Cheki kwenye Tribe43 ya #PEOPLEDAILY.

ODINAREH BINGWA AWATOA KIJASHO WAFOKAJI WA JIJI.

Image
Cheki kwenye Tribe43 ‪#‎ PEOPLEDAILY‬