Posts

Showing posts from February, 2016

TENDA WEMA UENDE ZAKO

Image
Dully melody ajipata kwenye wakati mgumu baada ya kusaidia msanii chipukizi wa jiji la Nairobi ambaye anajulikana kama STEADY J. msanii huyo steady j ambaye Dully alimsaidia kwa kumuhifadhi na malazi na mavazi, tu baada ya msanii huyo aliyeshindwa na hela za malipo ya studio Dully Melody aliamua kumwambie arudi kwao Nairobi kwa sababu lengo lake lilikuwa limebuma la kufanya collabo na Dully Melody. Msanii huyo ambaye kwa sasa anatumia nyimbo za Dully Melo dy akisema ni za kwake hata kwa mdundo nyimbo hizo ameweka kwa mdundo account yake. kwa sasa Dully Melody yupo kwenye mikakati ya kumwambia azitoe kwa mdundo account yake, lakini msanii huyo Steady J amesusia kuzitioa na pia kuna nyimbo mpya ambayo anapanga kurecord ambayo ni ya Dully melody. Melody anaomba msaada kwa mashabiki kumsaidia kutatua hio shida

INTRODUCING NEW HIPHOP ARTISTE IN COAST,, LYRICAL KING.

Image
Katika michakato yetu ya upekuzi wa burudani tulikutana na msanii wa kuchana anaetokea mombasa. Na tulipo muuliza safari yake ya mziki haya ndio aliyotuambia. "Mziki nilianza 2010 nikiwa kama dancer kwenye kundi la TALIBAN DANCE CREW. ilipofika 2013 niliingia katika studio za TEE hits na kuachia kibao changu cha kwanza kwa jina BADO HAWATAKI. ambacho kilipendwa na wengi hiyo ilinipa bidii ya kuwa naweza na sikukata tamaa hadi sasa niko na vibao vinne na vyote vinafanya vizuri bado kuna mengi makubwa yanakuja hivi karibuni" Lyrical king ndo jina lake la usanii naye anahitaji support yetu kufikia azimio lake la mziki

JE DULLY MELODY AKAFANYWA NINI??

Image
Baada ya dully melody kupost kwa wall yake"HAKI HII SIKUTARAJIA KUTOKA KWAKO MY BRO..IPO SIKU TU..NDO KUKOMAA" watu wa karbu walijawa na ghadhabu kujiuliza kuna lipi linaendelea ama limemkumba msanii huyo.Ikatulazimu kumtafuta Dully melody kujua kipi kina kula mwengine? Ijapo Dully melody hakutaka swala hili kusema ila kwa kumrai alitudokezea..na haya ndio aliyosema. "Mimi kama dully melody nko na mshauri wangu wa karibu ambae ni kama kaka yan gu.swala alilofanya bado sijawai tarajia kutoka kwake..hii ni baada tu yakunipia simu kwamba kuna show ambayo ilikua jumamosi 13/2/2016,show hio ilikua ni ya malipo ambayo ilikua kama show yangu ya kwanza kulipwa tangu kuanza mziki..basi ndugu yangu siku ilipofika ilibidi kuuliza malipo kama alipewa ama bado kaka yangu HANS MAHMOUD alisema amelipwa nilipotaka kujua ni kiwango gani alisema twende tutaongea mbele mbele,tulipofika mazeras kuelekea kaloleni ambako show hio ingefanyka nilitaka anipe hizo pesa japo 1000...

YOUNG NJITA AMSHIRIKISHA BEKA KWA WIMBO MPYA "SIWEZI JUTA."

Image
Huku wengi wakimzoea kwenye mtindo wa kuchana hardcore hiphop. Gwiji wa chocolate city Malindi ameamua kububujika kiasi na kushika mkondo mwingine wa muziki. Japo bado Kanzu ni mpya sheikh ni yule yule kama wasemavyo waswahili, hivyo basi Njita amezuka akiangusha vina vikali kwa michano ya kimahaba. Huku akimshirikisha msanii wa kike Beka, video yao ina mvuto wa kipekee na uhalisia wa hali ya juu unaoleta dhana ya kimahaba. Wimbo wenyewe kwa jina SIWEZI JUTA upo chini ya uandalizi wa studio iliyosimama kidete kuleta talanta zinazoshika moto kwa kasi, Malindi Records. Bila shaka tusitumie mate ilhali wino upo....tazama uhondo wenyewe hapa----------->>>>>>>>>

PRODUZA KHALID ADONDOSHA LISTI YA WAREMBO ALIOWAHI KUWA NAO!!!!!!

Image
Baada ya baadhi ya washika dau kumuingilia produza Khalid kwa usimamizi wake kwa mdada Sis-P, Khalid aliamua kutokimya na waziwazi alikuja juu kwenye kurasa yake ya facebook na kubumburusha maneno. Produza huyu mmiliki wa A MILLION RECORDS amekua kwenye chuma moto hivi majuzi kwa kusemekana kuwa amemuweka msanii Sis-P kinyumba mbali na kumsajili kwenye studio yake. Vilevile, project ya msanii wa hiphop kufanyiwa pr omo na project za bure imeleta tatanishi kwa baadhi ya washika dau. Khalid alitoa listi yake ya wachumba aliowahi kuwa nao; ni vile tu hakutaja majina manake yangelikua mengine sasa!!!  Tukitoa tu baadhi ya maneno aliyochapisha produza Khalid kwenye ukurasa wake wa facebook..... "Wanauliza kama Sis P ni mpenzi wangu? She is a woman, I am a man, she has a P**y I have a D**k, what's the big deal...? By the way, sijui kwa nini mnamuweka midomoni sana ilihali nimekuwa na mahusiano mengi ya kimapenzi na presenters wakike kuanzia Pwani FM, Bar...

MSANII ATIWA MBARONI KWA KUPACHIKA BINTI MIMBA!!!!!!

Image
Msanii tajika anayetokea Malindi alijipata taabani jana usiku baada ya kukamatwa na polisi kwa shtaka la kupachika binti ya watu uja uzito. Kiwanja, ambaye ni rapper tajika mkaazi wa Malindi alikumbwa na janga hili saa nne usiku pale familia ya binti huyo ilipojimwaya nyumbani kwake na polisi kibao. Kiwanja alibebwa hobela hobela hadi kituoni alipofungiwa na kuachiliwa asubuhi. Inakisiwa kuwa familia ya binti huyo ni wakwasi mno na hawakupendelea Kiwanja kuwa na binti yao.

BAADA YA KUBANDIKWA JINA LA "PRODUZA MPIGA BEAT ZA VIKEBE" TEE AZIDI KUNG'ARA!!!

Image
Ni mtayarishi wa hits kibao tu, moja ikiwepo KideKide iliyompa Dazlah na Produza wake Tee sifa teletele. Produza Tee amekuza vipaji si haba na bila shaka ni mmoja wa maproduza tajika hapa Pwani. Hata baada ya msanii fulani kusema kuwa Produza huyu hajui lolote ila kupiga vikebe tu; Tee amewashangaza wengi kwani kwa sasa kibao alichokitayarisha kwa jina Iyo kinafanya vyema. Kibao hicho kilichowaleta wasanii Jay A na Dazlah pamoja kimepanda chati kwa wiki mbili tu baada ya kuachiwa. Hivyo basi wadau kaeni mkijua mdharau biu hubiuka!!!

BAADA YA NAIROBI BARIDI SASA NI GOOD MORNING.

Msanii wa kizazi kipya Babu Dee Mapete ameachia kibao kipya kwa jina Good Morning ndani ya studio ya Morbiz Thunder Sound. Wimbo huu kwa sasa upo mtandaoni unaeza kuipata mkito kwa sasa nyimbo hii iko na ujumbe utamu wa mapenzi hasa wakati huu wa valentine pata utamu wa wimbo huu sasa. Babu Dee ameshukuru mashabiki wake kwa ushirikiano waliompa kwa wimbo wake wa Nairobi Baridi kwa sasa anaomba mupokee ujio huu mpya kwa mikono miwili.

MSANII CHANGEZ ALETA 'CHANGES' KWA JAMII.

Image
Msanii Changez Ndzai kutoka hapa pwani, ambaye licha ya kujihusisha na sanaa yeye pia anajihusisha na maswala ya kuridisha kwa jamii kupitia Shirika lisilo kua la kiserikali. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Changez amekua akiwatia moyo ama ku inspire vijana wengi kwa juhudi anazopiga kila uchao. Hadi kufikia sasa Changez ambaye anazuru shule za Kaunti ya Makueni, amekonyezea picha hii kuonyesha jinsi anavyopenda kuwa karibu na watoto ambao ndio hunufaika kwa sana kupitia miradi wanayotoa kwenye shirika.

INTRODUCING NEW ARTIST MICK PLANET.

Image
Mick planet ni msanii wa kizazi anaetokea jijini Malindi city. Amefanya nyimbo yake ya kwanza kwa jina Kilio changu ilioandaliwa ndani ya studio ya True Crazy mjini Malindi. Baada ya kutoa kibao hicho ambacho kipo kwa redio station za Pwani. Ameamua kuachia kibao kipya kwa jina Yalaiti alichokifanya kwa Produza Tee, wa Tee Hits Studio . Kibao hiki atakiachia wiki ijao kwa hio anaomba ushirikiano kwa washikadau wa mziki na mashabiki wampokee vizuri ilikuweza kufanikisha azimio lake.

Mr. Jojo Set To Release New Collabo With Shims & Aviva

Image
Burundian and Umuco Records CEO, "Mr. Jojo" is set to release yet another international collaboration titled Why, and this time he features Kenyan femcee "Shims" and singer, Aviva. This is coming just weeks after Mr Jojo Released new single titled Hello .

INTRODUCING DAVY GZE.

Image
Pwani Usanii: majina yako kamili? Davy Gze:majina yangu kamili ni David Haron Baraza mtoto wa mwisho katika familia yangu Pwani Usanii:watokea upande gani Davy Gze:naishi likoni Pwani Usanii:ulianza mziki lini? Davy Gze:nilianza mziki mwaka wa 2007 nikiwa shuleni japo nilikua sijarekodi. Pwani Usanii:ulirekodi lini.? Davy Gze:mwaka wa 2008 ndipo mwalimu mmoja aliridhika na nyimbo zangu nakuamua kunipeleka studio kurecord Flash Records ambapo nilifanya nyimbo yangu ya kwanza iliyowapa motisha watu kutaka kuskia nyimbo ya pili ila ilikua ngumu kama rasta bila msokoto kwani nilikua nasoma. Pwani Usanii: Je baada ya kumaliza masomo. ? Davy Gze:nilipomalza shule ndipo nilirudi kufanya kibao chini ya produza Nicky Wizzoh katika studio ya Wizzoh classic empire ambapo nilimshirikisha Sticky wa manabii tukafanya nyimbo kwa jina Siku Yangu Pwani Usanii:ulikarishwa vipi baada ya kutulia kwa muda? Davy Gze:nashukuru kwa wote wanaosupport kazi zangu akiwemo Kassim Mbui wa Pil...

HIVI JE SUDI BOY ALIPIGANA NA MSANII CHIPUKIZI KOFFI?

Image
Katika pitapita zetu mitandaoni,Tulikumbana na habari kuwa Sudiboy alishikana mashati na msanii wa Nairobi kwa jina Koffi. Japo picha zenyewe zilidhihirisha Ni video,habari hizi zimeinua hisia za mashabiki zake na inakisiwa kuwa tukio hili huenda likiwa la kweli.kisa hiki kinafuatia baada ya Sudi kutojitokeza ili kumalizia video ya wimbo aliokuwa ameshirikishwa. Wimbo wenyewe ulikuwa wa msanii chipukizi Koffi aliyekuwa amemlipa Sudiboy hela kibao kama inavyosema blog huyo. Juhudi zetu za kumfikia Sudi ziliambulia patupu ila tutawajuza pindi habari zikiwa full kipupwe!!!!Msikae mbali.

INTRODUCING NEW FEMALE ARTIST CRAIN NOTRIL.

Image
Pwani Usanii: majina kamili waitwa nani? Crain Notril:Fransisca Okelo Pwani Usanii: wafanya aina gani ya mziki? Crain Notril:Nafanya aina yoyote ya mziki ila kwa sasa nafanya RnB hip hop. Pwani Usanii: jina la nyimbo yako mpya ni lipi na umefanya studio gani Crain Notril: jina la nyimbo ni 'Baby come over 'na nimefanya Sauti Records jijini Nairobi Pwani Usanii: lengo lako kwa kazi yako ya uimbaji Crain Notril:Niko na nyimbo ambayo nitafanya Jungle masters na ndoto yangu ni kuwa msanii wa hip hop bora kenya 'kenyan Nicky' Huyu msanii ako na uwezo mzuri tumpe ushirikiano mwema maana anaweza.

KWA KUSUPPORT VIPAJI VYA PWANI; MUNGU HAKUKUSAU. KONGOLE MANUEL NTOYAI WA ‪#‎TRIBE43‬ NA ‪#‎SPICEMAG‬ PEOPLE DAILY!!!

Image

KAA LA MOTO LAWACHOMA MARAPPER WA JIJI KUU!!!!

Image
Tamasha la WHO IS KING likifanyika Wikendi hii na habari zinazotamba mitandaoni ni kuwa rapper Kaa La Moto aliyekuea anaiwakilisha pwani aliibuka kuwa bingwa wao kwa michano iliyosimama. Japo tamasha hilo halikuwa la freestyle battle, bali la kuvuta wingi wa mashabiki na kufreestyle topic yoyote unayopatiwa. Rapper Kaa la Moto ameamkia mitandaoni kupiga tarumbeta ya ushindi wake. La Moto aliandika haya...... "Nina Furaha sana mpaka n ashindwa na la kusema...We made it..You made it..I made it..Kwa maelezo zaidi ingia Twitter then ni follow @Kaa_moto au @Juliani au @jumpman wa Homeboys see what's trending kwa kuandika # Whoisking ...Au uliza MTU yeyote aliyefika # AllianceFrance jana ...Anyway it wasn't a BATTLE kama vipi wengi walitarajia,ila show ya Real emcees"Nani ana pull crowds, Nani ana freestyle any given topic on Stage na Nani ndio kusema?"... * Kaa La Moto Kiumbe going Live for the first time and He made it 100%. *Coast representative sai a...

RAPPER CANNIBAL AJIUNGA NA SIASA!!!

Image
RAPPER GWIJI ANAYETOKEA HAPA PWANI, CANNIBAL SHATTAH ATAWANIA KINYANG'ANYIRO CHA MCA KIEMBENI WARD 2017. JAMAA HUYO ALIYEKIMYA KIMUZIKI KWA SANA ATAKUWA AKIPEPERUSHA BENDERA YA ODM MWAKA UJAO.