Posts

Showing posts from 2017

MWINYI KAZUNGU (TOP MASHARIKI) AMSIFIA DULLY MELODY KWENYE INTERVIEW MPYA!!!

Image
MWINYI KAZUNGU (TOP MASHARIKI) AMSIFIA DULLY MELODY KWENYE INTERVIEW MPYA!!! Mtangazaji sifika Afrika Mashariki, Mwinyi 'Mtetezi' Kazungu wikendi iliyopita alidunda Pwani kwa kuandaa show kadhaa za kipindi chake cha Top Mashariki TV show kwa KBC. Mtetezi, katika pilka pilka zake alipata fursa ya kumhoji msanii Dully Melody katika maeneo ya Pirates beach na hapo ndipo aliposhuhudia kipaji cha mkali huyu kutoka Pwani. "Kusema kweli, Dully Melody ni mwenye kipaji si haba.Ni mara yangu ya kwanza kumfanyia interview na nimeona kipaji chake kitanawiri na mimi binafsi pia nitahakikisha dau Lake la sanaa laelea Juu. Nimekuza vipaji vingi vya Pwani na Dully bila shaka amenionyesha anao uwezo."Alidokeza Mtetezi. Presenta huyu ambaye yupo mstari wa mbele kwa kuenua vipaji vipya si Pwani pekee bali Kenya nzima aliongeza kwamba atarudi Pwani kuja kufanya show zaidi za kipindi chake cha Top Mashariki kwani huku ndiko kwenye chimbuko halisi la vipaji vinavyoibukia. Kwa mengi...

ONE ON ONE WITH RICKY BEKKO.ONE OF THE BEST VIDEO DIRECTOR IN KENYA.EXCLUSIVE INTERVIEW!!!!

Image
LIGHTS, CAMERA, ACTION!!!! JUST SIX QUESTIONS FOR RICKY BEKKO. 1.What's your government names? RICKY :My government names are Ricky Bekko but a lot people think its an industry name not unless they send Mpesa or do any formal business that require signing of documents. 2.Did you ever dream of being a video Director/producer? RICKY :Actually, not growing up i never knew what i want to be but i would have been a lawyer if I had the chance to go to campus but our family wasn't well off. So in the process of hanging out with my friends who were musicians and seeing their struggle of shooting videos thats how i slowly ventured into this industry. 3.Which schools did you attend? RICKY:I went to Mariakani primary school and did my kcse in Good Samaritan High school in Kawangware that was it. The rest was what i call school of had knocks thats where you learn to survive through each means. I used to sell water, simcards, i was once a waiter in a local hotel and mo...

DOGO RICHIE ANIHARIBIA BIASHARA KWA KUTONGOZA WASANII WA KIKE WAKIJA STUDIO--PRODUZA AMZ ATOBOA SIRI!

Image
DOGO RICHIE ANIHARIBIA BIASHARA KWA KUTONGOZA WASANII WA KIKE WAKIJA STUDIO--PRODUZA AMZ ATOBOA SIRI!!! Idadi ya wasanii wa kike ndani ya studio za Tempoz imepungua sana jambo lililomfanya Produza Ammz kuongea. Jambo hili limeleta ugonganishi kati ya studio ya Tempoz na msanii Dogo Richie kwani yasemekana kuwa msanii huyu ana tabia ya kuwatongoza wasanii wa kike pindi wanapokuja studio. Dogo Richie kwa sasa, kama tulivyobaini ametongoza zaidi ya wasanii sita wa kike na kuwadanganya kuwa atapiga nao kolabo na kuwashika mkono kimuziki ili waweze kujulikana kwa urahisi. Jambo hili ndilo lililomkera produza Amz ambaye vilevile ni mmiliki wa studio hiyo. Amz alisema ya kuwa jambo kama hilo linamuharibia biashara na hadhi yake kama produza. "Wasanii wote wa kike wameacha kuja studio na pia idadi ya customers wangu wa kike pia imepungua tangu Dogo Richie akinyage studio. Tabia kama hizi ndogo ndogo ndizo zinazokandamiza sanaa ya Pwani na kupoteza vipaji vya mabinti bure. Nimejaribu...

UKINIJIBU NAKUROGA - - - KAULI YA SUSUMILA KWENYE WIMBO WAKE MPYA TEBWERE download it here!!!

Image
Msanii mkali tokea Pwani, Susumila amezuka tena na disstrack kali sana. Susumila baada ya kutajwa na msanii Dogo Richie kwenye nyimbo ya majanga, msanii huyu wa Tuliza Nyavu ameachia kibao chake huku akitoa misemo mikali... "Majanga ni msanii kuishi nyumba ya tenga mbili....." Akiongeza msumari Moto kwenye kidonda jamaa huyu wa Wachawi international alimalizia kwa mistari kuwa msanii yeyote atakayejibu diss hii yake atamroga. Haya nani yuataka kurogwa!!???? Ipakue nyimbo yenyewe hapa >> http://mdundo.com/song/97049

MSWAZI MASAUTI KUMBE KASAJILIWA NAIROBI TENA!!!!!

Image
MSWAZI MASAUTI KUMBE KASAJILIWA NAIROBI TENA!!!!! Msanii wa miondoko ya swahili RnB Mswazi Masauti amezuka tena baada ya kimya Kirefu. Meza yetu ya habari imebaini kuwa jamaa huyu baada ya kuwachana na Lebo ya Swarnb alipokuwa amesajiliwa chini Ya produza Ted Josiah, Mswazi amesajiliwa chini ya studio zilizoko Nairobi. Kwa mara nyingine tena,msanii huyu wa kibao cha 'Mahabuba' ameweka guu lake ndani ya jiji kuu la Nairobi na kupata fursa ya kufanya kazi chini Ya usajili wa Melwood studio ambapo atafanya kazi Na produza anayebobea, Motiff. Produza huyu amefanya kazi na wasanii kama Khaligraph Jones, The Kansoul na wengineo. Baada ya mawasiliano na msanii huyu, Masauti alidokeza kuwa kuna ngoma nyingi tu ambazo amefanya na hivi karibuni zitawachiliwa rasmi.

KILA MTU NA MSIMAMO WAKE NDIO SANAA INAVYOENDA ASEMA PRODUZA AMMZ

Image
KILA MTU NA MSIMAMO WAKE NDIO SANAA INAVYOENDA ASEMA PRODUZA AMMZ Produza na mmiliki wa studio za Tempoz, produza Ammz Jadidi au Tone la Maji ametoa kauli yake kuhusiana na maoni yatolewayo kuhusu sanaa. Haya yote yanajiri baada ya maswala kadha wa kadha kuibuka, yakiwemo show ya msanii Tekno Miles iliyobuma na Anita Santuri wa Pwani Celebrity Awards kusuta Cartels za muziki wa Pwani. Ammz amekuwa muwazi sana na kusema kuwa kila mmoja huwa na msimamo wake dhabiti anaouamini. Pasi kupoteza muda Soma alichonakili produza huyo hapa.... "Nimekuja kugundua hapa Kenya usiwahi kubishana na mwenzako kuhusu sanaa ya mziki inavyopaswa kuendeshwa. Kwa sababu kila mtu anajua na anaamini kila "point" anayoitoa. Washikadau wako na misimamo mikali wanayoiamini pa kubwa sana. Tatizo ni kuwa misimamo hii inatofautiana kutoka kwa mshikadau mmoja hadi mwengine. Na endapo utalazimisha kubadili msimamo wa mtu basi huenda ukajijengea chuki na huenda ukaharibu hata kazi yako. Hali hii i...

ANITA WA PWANI CELEBRITY AWARDS AGADHABISHWA NA CARTELS ZA MUZIKI PWANI!!!!!

Image
Anita Santuri, ambaye wengi wetu twamfahamu kupitia tuzo za Pwani Celebrity Awards na Ashantyz promotions amegadhabishwa sana na tabia ya washika dau wa sekta ya muziki pwani. Mwanadada huyu ambaye pia ni Mtangazaji wa kipindi cha Mseto East Afrika cha Citizen TV aliyatoa maneno haya tarehe 9,mwezi wa Septemba huku akilalamika sana kuwa wasanii wanaoibukia hawapewi nafasi kwa sababu jamaa wamejenge Vikundi vya kivyao vyao ili wajipe support wao kwa wao. Anita alipachika haya kwenye Facebook.... "I'm so disappointed at some of the coast entertainment stakeholders. .... why not support? ?? why not give chances to talents?? why create a crew that is enclosed not allowing change? ?? is it coz you think the other person will outshine you? but that's how you create healthy competition yawa..... then unakaa kwa TV ukisema vile umesaidia watu wengi!!!!! really !!!!!!! anyways tushawazoea. bora uzima hata nyerere na moi walikua raisi hivi wamestaafu..... UTASTAAFU PIA. ........

RAPPER WA KIKE TOKEA PWANI AWACHIA PINI JIPYA!!!

Image
RAPPER WA KIKE TOKEA PWANI AWACHIA PINI JIPYA!!! Idadi ya wasanii ikizidi shuka hasa hapa Pwani, msanii wa kike anayetamba kwa mtindo wa hiphop, Boomer Best amekuja vikali kwa video mpya. Boomer Best aliye chini Ya Young Boss music alipiga wimbo hatari kwa jina 'Mtoto wa Kike' na video kufanywa na Director Lamar. Video hiyo yapatikana kwenye you tube. Icheki hapa.... ameweza? https://youtu.be/ZPKx9vZBXmo

TAZAMA VIDEO YA MSANII BEKA THE BOY KUTOKA KENYA

https://youtu.be/JNmNKyoRmcM

WEZI WAJIPATA UCHI WA MNYAMA BAADA YA KUIBA GARI. BAMBURI MOMBASA

Image
Habari zinazotufikia kwa sasa ni kwamba wezi wawili wa gari maeneo ya Bamburi, Mombasa walijipata taabani pale walipoiba gari na mambo yao kuwaendea mrama. Kalameni hao wawili, walijipata uchi wa mnyama na kuchezea chezea matope huku wakidandia dandia gari hilo. Baadhi ya umbea uliotanda mitandaoni, ni kwamba wawili hao waliletewa mganga mganguzi na kuwafanyia vimbwenga hivyo. Wengine wanadai ya kuwa gari hilo lilikua limefungwa kupitia nguvu za Kiafrika hivyo basi anayeliiba bila shaka hujipata hali si hali. Tazama picha.....

SIRI YA MSANII HUYU KUANDAA VIDEO YAKE NDANI YA NYUMBA YA TYCOON FLANI WA KENYA YAFICHUKA!!!!

Image
SIRI YA MSANII HUYU KUANDAA VIDEO YAKE NDANI YA NYUMBA YA TYCOON FLANI WA KENYA YAFICHUKA!!!! Pilka pilka zikizidi pamba moto kisiasa, wasanii wa Kenya wameamua kutosubiri moto huu kuzima. Jambo hili ndilo lililomfanya msanii anayeibukia vizuri kutoka Kenya, Beka the Boy kuingia ndani ya nyumba ya mchoraji sifika duniani Giampaolo Tommasi ili aweze kutengeneza video yake. Hivi je kusudio lake kuu lilikua lipi? Meza yetu ya habari ilibaini kuwa msanii huyu alitaka kupata picha na mvuto wa tamaduni tatu tofauti zikiwemo Swahili, Giriama na Italiano. Nyumba ya jamaa huyo, Giampaolo Tommasi imepambwa kwa picha za kuvutia zinazoleta tamaduni zote tatu pamoja hivyo basi mshikamano na maana fiche zimebebwa vyema kabisa kwenye mandhari haya. Je video ya wimbo wenyewe ni ipi? Ni swali wanalojiuliza wengi wa mashabiki. Tukizipunguza dukuduku zenu, wimbo wenyewe wajulikana kama "Jidai" uliotayarishwa na produza Totti La Inter na video imetayarishwa na produza anayebobea sana kw...

JE JAFFARIZOH KAWACHA MUZIKI NA KUWA VIDEO DIRECTOR??? PATA UKWELI HAPA!

Image
JE JAFFARIZOH KAWACHA MUZIKI NA KUWA VIDEO DIRECTOR??? PATA UKWELI HAPA! Huku akibandika picha hizo kwenye kurasa zake za Facebook, Ryzo huandika na kupiga Lebo picha zake kwamba kampuni yake ya video ni ANOTHER LEVEL FILMS. Ni majuzi tu pale alipobandika picha na kudai kuwa ana wimbo mpya ulioandaliwa na produza Morbiz na video chini Ya kampuni yake ya Another Level Films. Huku akibandika picha hizo kwenye kurasa zake za Facebook, Ryzo huandika na kupiga Lebo picha zake kwamba kampuni yake ya video ni ANOTHER LEVEL FILMS. Ni majuzi tu pale alipobandika picha na kudai kuwa ana wimbo mpya ulioandaliwa na produza Morbiz na video chini Ya kampuni yake ya Another Level Films.

SANAA YA PWANI :BEKA THE BOY TAYARI KUWACHIA KIBAO KIPYA MTINDO WA RnB.

Image
SANAA YA PWANI :BEKA THE BOY TAYARI KUWACHIA KIBAO KIPYA MTINDO WA RnB. Sio mtindo uliozoeleka na wengi bali msanii akiufanya basi lazima watu watulie wasikilize. Beka the Boy ameamua kufanya mtindo wa RnB kwenye wimbo wake mpya Jidai. Chini ya uandalizi wake produza gwiji pwani, Totti La Inter, Beka amewachia vokali safi na za kuteka nafsi za wapenda muziki. Video imetayarishwa ndani ya Malindi city, director akiwa Marvin Brudaz wa Undepicted Films and photography. Uzinduzi wa video utafanyika Malindi Fermento 9 September 2017 from 11:00. Kwa sasa tusidokeze mengi ila tusubiri video yenyewe.....