WASANII WENGI WA PWANI HUKIMBILIA KAZI ZA UARABUNI KISA MUZIKI WA PWANI HAULIPI!!!(part one)
Sanaa ya pwani hukumbwa na matatizo kila uchao. Kila siku na tatizo lake mpya. Jambo hili limeifanya sanaa ya muziki hasa pwani kuwa ngumu na vijana wanaofanya muziki kama ajira wanaambulia wanaambulia patupu.
Muziki kama biashara ni mithili ya kukamua jiwe litoe maji,jambo lililopelekea wengi wa wasanii kutafuta ajira ng'ambo.Ng'ambo hii si nyingine bali nchi za Uarabuni au ukipenda 'Middle East' kama wenyewe wakuitavyo.
Sehemu mbali mbali za Uarabuni kama vile Dubai,Qatar,United Arab Emirates,Pakistan, Abu Dhabi,Iran na nyinginezo zimepokea 'wasanii' wengi hivi majuzi.
Hivi je tatizo ni lipi?Tuliwasiliana na msanii wa hapa Pwani kwa jina MnS (wa HalfBouncy clique) akatueleza haya,"Mwanzo kabisa,muziki hauwezi kamwe kuchukuliwa kama ajira pwani.Kwa sababu sanaa ya pwani bado haijakomaa na pindi utumiapo pesa zako kujiendeleza kimuziki basi hazikupi faida kamwe ndiposa wengi Wetu tumeamua kutafuta riziki huku Uarabuni."
Baadhi ya washika dau waliokimbilia Uarabuni kusaka "greener pastures" ni kama MnS, Sketcher wa kundi la Rudeboys,Renny Blazer,Kim wa Lavichunare,Mchizen Pator wa G-Block Makini, na wengine wengi.
Sio wasanii pekee bali hata maproduza tajika na dancers vilevile wamekimbilia Uarabuni kusaka maisha.......(PART ONE)
SUBIRINI PART HIVI KARIBUNI....
Comments
Post a Comment