HII SASA KALI!!! OTILE BROWN KAIBA AU KATOROKA NA LAPTOP YA WENYEWE??
Msanii aliyeenuka kwa kasi Afrika Mashariki,Otile Brown hapo Jana Jumatatu 3/10/2016 aliwashangaza wasikilizaji wa Radio Maisha asubuhi kwenye kipindi cha MAISHA ASUBUHI Kinachopeperushwa hewani na watangazaji Jalang'o na Alex Mwakideu.Kwenye kipindi hicho kuna kitengo cha kumpigia mtu simu na kumwambia alipe deni la mtu hasa kama huyo jamaa amechelewa kulilipa.
Watangazaji hao wawili walipokea simu ya kutatanisha ya jamaa flani Kutoka mitaa ya Mikindani,Mombasa aliyedai ya kuwa Otile Brown ni rafiki yake wa zamani na alimkabidhi laptop yake na Otile akaingia nayo mitini mpaka Leo.
Kilichofuata ni watangazaji hao Alex Mwakideu na Jalas Mwenyewe wa Radio Maisha kumpigia msanii Wetu anayevuma kwa kibao chake kipya PAKATE ili wajue ukweli na ikiwezekana msanii huyo msahaulifu alipe laptop aliyotoroka nayo.Msanii wetu,Supastar Kanjanja aliposhika simu na kuulizwa kuhusu Laptop hiyo,alizima simu 'faster faster' na kuwa mteja siku nzima!!!!!!!!!!!!
Comments
Post a Comment