VIDEO YA MSANII YAPIGWA VITA BAADA YA KUMTUMIA MKE WA WENYEWE.
Hivi majuzi kulipamba moto baada ya msanii kufuatwa hadi nyumbani kwake na familia ya dosi Fulani.
Msanii huyu almaarufu BMG,alipigwa na bumbuazi pale watu watatu walipomfuata hadi nyumbani kwake kutaka kujua ni vipi alifanya video na mke wa watu.
Video hiyo ya wimbo wake 'Chikera' yasemekana aliyekuwa video girl ni mke wa mtu,tena wa harusi haswa. Mumewe video girl huyo alikua na hamaki na kwa kuwa yupo na uwezo mkubwa kifedha ameamua kuibania video hiyo kuchezwa vituo vyote vya runinga.
BMG aliyesajiliwa na Grip music and Pictures aliandaa video hiyo hivi majuzi hapa Kenya na nchi ya German pia.
Tulipowasiliana na BMG alitueleza kuwa yupo katika pilka pilka za kutuliza mambo yote na video itakuwa hewani muda wowote kuanzia saa hii.
Juhudi zetu za kuwasiliana na video girl tajika hazikufua dafu ila pata kumuona video girl mwenyewe hapa na jinsi mambo yalivyojiri.........
https://youtu.be/e-2olrsJGmk
Comments
Post a Comment