MWANADADA MNIGERIA ATAKAYESISIMUA VIDEO YA FRANKIE DEE!!!!


Huku kibao chake kipya cha Madda dem kikizidi kupata makali,staa wa miondoko ya dancehall Frankie Dee yasemekana ana mipango bambam ya video.
Frankie Dee ambaye vilevile ni mmoja wa watumbuizaji wa tamasha la Msanii Romain Virgo,kupitia kurasa za Dancehall Msa Family and Friends ilisomeka kuwa jamaa huyu atatoa video na vide vixen mashuhuri anayetokea Nigeria.

Video hiyo itakayoandaliwa na video director X-Antonio amepigiwa debe kuwa itakuwa moja ya kipekee na itakayoleta mageuzi kwenye sanaa ya Afrika Mashariki.Japo haikuwekwa wazi wimbo upi utakao fanyiwa video hiyo,tuna imani kuwa Frankie Dee atawasha moto kwenye ulingo wa muziki wa Afrika Mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA