SAUTI MPYA MJINI; PATA KUMFAHAMU MSANII LA TWKUL
Alianza muziki mwaka huu na kamwe ameamua kutorudi nyuma.Msanii La Twkul amejitosa kwenye maji ya kina kirefu na ana imani kuwa nyota yake itan'gaa.
La Twkul aliandaa nyimbo yake ya kwanza 'chekecha' akiwa katika kundi la Wapole Band.
Baada ya kundi lake la Wapole Band kusambaratika,LaTwkul aliamua kuanza kufanya muziki kivyake kama solo artist.
Kwa sasa kibao chake kipya kinatoka tarehe nne mwezi huu. Kibao chenyewe 'niokote' kimeandaliwa Asali records chini ya produza B.i.
La Twkul alituelezea kuwa lengo lake kuu kwenye muziki ni kuwa Msanii wa kipekee atakaye kuwa kielelezo kwa jamii na kuigwa vizazi vijavyo.
Comments
Post a Comment