KUTANA NA SAYARI ZEDDY AKITAMBULISHA NYIMBO MPYA.
Ukisikia flavour za pwani basi hutokosa kumtaja Sayari Zeddy. Msanii huyu anayetamba kwa nyimbo yake DEDE ni mwenye kipaji na kuleta utamaduni wa pwani kwa fleva zake zilizokolea maudhui na sifa za pwani.Tuliwasiliana naye kupitia njia ya simu kuhusiana na wimbo wake mpya na Zeddy alikua na haya ya kutuambia.......
"Hi ni ngoma yangu ya tisa.
Nilifanya ngoma yangu ya kwanza Bigfoot Production ambayo yaitwa (Moyoni) Kisha nikafanya, Hayana siri, Nakutafuta, Heshima na 'Laiti ungejua' niliyoshirikishwa na dogo anaitwa GWIJI R. Zote hizo ni Tee Hits Production. Kisha nikarudi Bigfoot nikafanya 'Niko naye'. Ngoma ya saba ni 'Tosheka' ambayo niliifanyia Jungle masters Production. Kisha nikafanya 'Dede' ndani ya Green house kabla ya hii mpya sasa inayoitwa 'Kusudi'."
Nyimbo kusudi aliyoifanyia Greenhouse production ndio anayoitambulisha kama kazu yake ya msimu huu wa sikukuu.
Comments
Post a Comment