Ni msanii aliyekubalika na wengi na aliyevuma kwa vibao motomoto kama; mtoto wa shule,umaskini si kilema,kadem,toka nenda,kadem kameparara na nyinginezo. Msanii huyu aliyemaliza shule ya upili mwaka uliopita alifuzu na kuchaguliwa kwenye kikosi cha askari polisi kitengo cha AP. Ranny aliyekuwa studio ya Homeworks na kuhamia studio ya Mwamba records kwa sasa yupo kwenye kambi mafunzoni na aliahidi kuwa kamwe hatowacha muziki,atashughulika na muziki pamoja na kazi yake mpya ya kulinda usalama.
Comments
Post a Comment